*Dk.Mwakyembe awaambia wabunge kwa sasa wanahojiwa,kisha mahakamani

Na Ripota Wetu,Dodomma

MSANII nyota katika muziki wa kizazi kipya maarufu Bongo Fleva nchini Nassib Abdul a.k.a Diamond amejikuta akiwa kwenye mikono ya Jeshi la Polisi ambapo kwa sasa anahojiwa kutokana na kusambaza picha chafu mtandaoni.

Akizungumza mjini Dodoma bungeni leo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Harrson Mwakyembe amewaambia wabunge Diamond amekamatwa jana na sasa anahojiwa Polisi na baada ya hapo atafikishwa Mahakamani.

"Naomba nitoe taarifa kuna baadhi ya wasanii wetu walianza kufanya uhuni uhuni ndani ya mitandao.Jana tumemkata msanii nyota Nassib Abdul na kumpeleka Polisi na sasa anahojiwa kutokana na picha ambazo amezungusha mtandaoni.

"Pia Nandy naye apelekwe Polisi na tunaangalia namna ya wote kuwapeleka mahakamani,"amesema Waziri Dk.Mwakyembe wakati anawaambia wabunge kuhusu hatua wanazochukua kulinda maadili ya nchi yetu.

Amewataka vijana nchini kutambua mitandao si Kokoro la kupeleka uchafu wote mitandaoni na wafahamu nchi hii ina sheria zake na lazima zilindwe.

"Vijana wawe makini na matumizi ya mtandao ,hii nchi ina maadili yake na wote watakaosambaza picha chafu na mambo mengine yasiyozingatia maadili tutachukua hatua,"amesisitiza  Dk.Mwakyembe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...