Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
IMEELEZWA watu pekee wanaoweza kumaliza migogoro ya ardhi
nchini ni pande mbili ambazo zipo kwenye mgogoro na si
vinginevyo na hata watalaam wanapokwenda basi ni kwa ajili ya
kuweka mipaka tu.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Halmashaui ya Wilaya ya
Morogoro, Kibena Kimu wakati wa ufunguzi wa mdahalo wa haki za
ardhi wilayani Morogoro uliondaliwa na Shirika la mradi la PELUM
Tanzania.
Mdahalo huo unaofanyika kwa siku mbili na kushirikisha vijiji
vitano vya Mikese Lubungo, Newland na Mfumbwe vya wilayani
humo ambapo Kimu amefafanua haiweze kumaliza siku bila kupata
taarifa ya mgogoro wa ardhi kutoka kati ya wakulima na wafugaji
au kijiji na kijiji, kuhusu mipaka.
Ambapo kila mmoja anakidai kuingiliwa na mwenzake na hata
watalaamu wakienda na GPS wanakuwa na wakati mgumu
kutatua mgogoro huo.
"Nimekuwa nikiwashauri wakae pande zote mbili zinazolumbana
kuhusu ardhi na wanapokubaliana inakuwa rahisi kumaliza
mgogoro na watalaam wa ardhi wanakuwa sehemu ya mashahidi
tu,"amesema.
Ameongeza elimu inayotolewa na PELUM kuhusu kutambua
rasilimali ardhi na namna gani ya kumiliki na kuwa na uwezo wa
kushughulikia migogoro ya ardhi inayojitokeza imesaidia sana
wananchi.
"Kwani vijiji vyote vina mabaraza ya ardhi lakini elimu waliyopata
pengine haijatosheleza.
Nawashukuru PELUM kwa kazi
wanayofanya na elimu wanayotoa ya kusimamia matumizi bora ya
ardhi kwenye halmashauri yetu ya Morogoro.
"Rasilimali pekee tuliyonayo watanzania ni ardhi kitu ambacho nchi
zingine hakipo.Tumeona ujio wa watu wengi wakija kwa ajili ya
kuchukua na kumiliki na kuwekeza kwenye miuondombinu ya ardhi
yetu, tusipokuwa na uwezo wa kumiliki ardhi, tunaweza kuja kuwa
watumwa kwenye nchi yetu,"amesema.
Amefafanua watu wanaendesha maisha yao kwa kilimo na hali ya
kawaida na kusisitiza mpango unaofanywa na PELUM wa
kuwapimia vipande vya ardhi wananchi wa kawaida na
kuwatengenezea hati miliki za kimila ni jambo la msingi.
"Hati hizo za kimila zitawawezesha wananchi kwenda kukopa na
kuenedeleza au kuwekeza kwenye maendeleo yetu na kutengeneza
viwanda vidogo.
"Hata pale wanapokuwa na changamoto za mvua na bei ya mazao
basi wanaweza kuyafanya kuwa mazao ghafi na kuyatunza katika
ubora mpaka pale yatakaposafirishwa,"amesema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...