Ahadi hiyo imetolewa mjini hapa leo na Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia walipozungumza na waandishi wa habari kueleza utekelezaji wa hoja za CAG katika sekta zao.

  Waziri Ummy: Tunakagua Deni la Wagonjwa Nje

Akieleza utekelezaji wa hoja mbalimbali katika sekta ya Afya, Waziri Ummy ameeleza kuwa Wizara ya Afya, baada ya kupata taarifa ya CAG kuhusu kuongezeka kwa deni la matibabu ya wagonjwa wanaopata rufaa nje ya nchi, imeamua kufanya uchunguzi wa kina wa kitabibu na kihasibu kujua usahihi wa deni hili ili kuchukua hatua madhubuti.

Aidha, amesisitiza kuwa Wizara imekubaliana na ushauri wa CAG wa kuhakikisha Serikali inaendelea kuboresha utoaji wa huduma za kibingwa hapa hapa nchini nchini ili kupunguza gharama. Waziri Ummy ameeleza hatua mbalimbali zilizochukulia kutekeleza agizo hilo ikiwemo kuanza kutolewa hapa nchini huduma za upasuaji wa moyo, upandikizaji wa figo, uwekaji wa vifaa vya usikivu na matibabu ya magonjwa ya mifupa na mishipa ya fahamu.

Kwa upande wa huduma za kibingwa katika maradhi ya saratani, Waziri Ummy alisema tatizo kubwa lililopo sasa ni huduma za kiwango cha juu cha kupima ugonjwa huo ambazo hazipatikani sehemu nyingi za Afrika. Hata hivyo alisema katika mwaka mmoja ujao Tanzania itamaliza tatizo hilo kwani Serikali imetenga Shilingi bilioni 14.5 mwaka ujao wa fedha kununua mashine ya kupima saratani (PET-CT-SCAN) 
.
Kuhusu uingizwaji wa bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 1.94 kwa kutumia vibali vya kughushi, Waziri Ummy amesema wameshachukua hatua za haraka kupitia Bodi ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuwabaini wote waliohusika na tayari baadhi wameshakabidhiwa kwenye vyombo vya dola huku TFDA ikichukua hatua za kujiunga na mfumo wa TRA ili kutambua nyaraka zisizo halali.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akijibu hoja zilizotolewa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za  Serikali (CAG)kwa mwaka wa fedha unaoishia june 2017. Mapema leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia,  Prof. Joyce Ndalichako akitioa maelezo kuhusu kuhusu mafanikio ya Wizara hiyo hasa katika ukusanyaji wa mikopo iliyoiva kwa wanafunzi wa elimu ya juu wakati akijibu  hoja zilizotolewa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za  Serikali (CAG)kwa mwaka wa fedha unaoishia June 2017. Mapema leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari kabla yakuwakaribisha Mawaziri kushiriki katika mkutano na Waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu hoja mbalimbali zinazogusa Wizara zao katika ropoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka unaoishia June 2017.
Serikali imesisitiza kuwa hakuna hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika sekta zote na hususani sekta za Afya na Elimu ambayo haitatekelezwa ili kuhakikisha azma ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafikiwa ipasavyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...