Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

MKOA wa Dar ea Salaam umeadhimisha miaka 54 ya Muungano kwa kutoa misaada ya chakula na malazi kwa familia zilizoathiriwa na mafuriko yaliyotokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni.

Akizungunza leo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema misaada iliyotolewa ni pamoja na magodoro, chandarua, nashuka, mito, sukari, unga,mchele pamoja na mafuta ya kupika.

Makonda amesema misaada hiyo itagawanywa kwa familia zaidi ya 600 zilizoathiriwa na mafuriko lengo likiwa ni kusaidia familia hizo ambazo zimekuwa zikiishi kwa tabu baada ya mvua kuharibu vyakula na mali.

Aidha amezishukuru taasisi za Abdullah Aid na Miraji Islamic Center kwa kuamua kutumia maadhimisho ya muungano kugusa maisha ya familia zilizokuwa zikiishi kwa tabu.

Pia amesema kuwa Mkoa umeandaa mkakati wa kukabiliana na mafuriko ya mara kwa mara ambapo hivi karibuni atahitisha mkutano na wananchi wote waishio mabondeni ili kuangalia namna bora kutatua suala hilo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa taasisi ya Miraj Islamic Center Abdullah Mrus na Mwenyekiti wa taasisi ya Abdullah Aid Arif Ally Abdurahman wamesema wameamua kutumia siku ya muungano kuzikumbuka na kusaidia familia ambazo zimekumbwa na mafuriko na sasa zinaishi kwa tabu.

Aidha wamempongeza Rais Dr. John Magufuli kwa kudumisha amani na mshikamano miongoni mwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda (kushoto) akipokea msaada wa chakula na malazi kwa familia zilizoathiriwa na mafuriko kutoka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya Miraj Islamic Center,Abdullah Mrus na Mwenyekiti wa taasisi ya Abdullah Aid Arif Ally Abdurahman leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza leo katika hafla ya kupokea msaada.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwashukuru viongozi wa taasisi za Abdullah Aid na Miraji Islamic Center kwa kuamua kutumia maadhimisho ya muungano kugusa maisha ya familia zilizokuwa zikiishi kwa tabu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi za Abdullah Aid na Miraji Islamic Center leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...