Balozi wa Tanzania nchi India Mhe. Baraka Luvanda ametembelea na kuhudhuria hafla ya wanafunzi wa Kiafrika wanaosoma kozi mbalimbali katika vyuo jimboni Punjab.
Hafla hii iliofanyika Mei18, 2018 ilijumuisha wanafunzi karibu wote wa Kitanzania wanaosoma Punjab. Ilijumuisha vyuo kama Gian Jyoti institute of management and technology( chuo kilichoandaa event) ambacho ni miongoni mwa vyuo bora vya masomo ya biashara nchini India, CDac na vyuio vinginevyo.
Hafla iliandaliwa na mwanafunzi Bakari Chuma wa mwaka wa pili anaesomea course ya MBA akishirikiana na uongozi wa chuo Gian Jyoti Institute of Management and Technology.
Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Baraka H. Luvanda wakiwa na mwambata wa elimu Bw. Yahaya A Mhata, Mwenyekiti wa Gian Jyoti groups of institutions Bw. J. S. Bedi na Dean wa wanafunzi wa kimataifa Gurdeepak Singh na baadhi ya wanafunzi wa Kitanzania Mariam Sunday na Vivian Omar na wengine kutoka mataifa mbalimbali.
Balozi Luvanda akiwa katika kilemba cha asili akikaribishwa na wenyeji
Balozi Luvanda akiwa ndugu Yahaya A Mhata pamoja na Mr j. S. Bedi chairman na Mkurugenzi Dr Aneet (saree ya njano) wakifurahi na wanafunzi
Balozi akiwa na wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Punjab.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...