Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

RAIS  wa Mali Ibrahim Boubacar Keita amempongeza kijana Mamoudou Gassama (22) aliyemwokoa mtoto aliyenusurika kuanguka kutoka ghorofani na kumtaka arejee nchini Mali kwani ameandaliwa kazi ya jeshi.

Akizungumza na vyombo vya habari balozi wa Mali nchini Ufaransa ametoa pongezi kwa kijana huyo kutoka kwa Rais wa Mali na kumtaka arejee nchini kuendelea na kazi ya jeshi aliyoandaliwa.

Aidha Mamoudou ameonekana akiwa na maafisa wa jeshi la zima moto la nchini Ufaransa akipata  mafunzo na kufanya baadhi ya shughuli katika kikosi hicho.


Ikumbukwe kuwa mapema jumamosi wiki iliyopita kijana raia wa Mali Mamoudou Gassam (22)  alifanya kitendo cha kishujaa cha kumuokoa mtoto mdogo ambaye alitaka kudondoka kutoka jengo la ghorofa ya nne, na baadaye kukutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kupatiwa zawadi nono, ikiwemo hati ya uraia wa nchini Ufaransa na nafasi ya kazi katika jeshi la zimamoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...