Na Ripota Wetu, Globu ya jamii.

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imetoa amri ya muigizaji Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela sasa atumikie adhabu hiyo kwa kifungo cha nje.

Hivyo kuanzia sasa Lulu amebadilishiwa adhabu na anatumia kifungo hicho akiwa uraiani na tayari Jeshi la Magereza limethibitisha kupokea amri hiyo ya Mahakama Kuu. Akizungumza kwa njia ya simu na Michuzi Blog iliyotakaka kupata ukweli wa taarifa hizo, Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es salaam, Naibu Kamishna wa Magereza Augustino Mboje amethibitisha ukweli wa taaarifa za Lulu kubadilishiwa kifungo hicho na kusisitiza hiyo imetokana na amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania.

"Ni kweli ndugu zetu wa Michuzi Blog, Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa amri hiyo na hivyo Lulu atatumia adhabu ya kifungo cha nje badala ya kukaa jela.Taarifa rasmi kuhusu Lulu tutaitoa kwa vyombo vya habari hapo baadae kwani tunaendelea kuiandaa lakini kwa kifupi,"amesisitiza Mboje.

Akifafanua zaidi  Mboje ni kwamba ieleweke Lulu  bado ni mfungwa wao na angeendelea kukaa jela hadi Novemba 12 mwaka huu ili kifungo chake kimepunguzwa kwa msamaha wa Rais. "Rais amempunguzia moja ya sita ya adhabu ya kifungo chake kwani ilikuwa atoke Machi 12 mwaka 2019."

Kwa kukumbusha tu Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kutiwa hatiani kwa kuua bila kukusudia msanii mwenzake Stiven Kanumba(marehemu).Kanumba alifariki saa nane usiku, mwaka 2012 baada ya kutokea mzozo kati yake yake na Lulu ambaye inaaminika walikuwa na uhisiano wa kimapenzi. Hivyo kitendo cha Mahakama Kuu ya Tanzania kutoa amri ya kubadilishiwa adhabu Lulu ya kutumia kifungo chake nnje kinatoa fursa kwake kupata auheni ya adhabu hiyo.

Kwa mujibu wa Jeshi la Magereza ni kwamba hivyo Lulu atatumikia adhabu yake kwa kupangiwa kazi za kufanya za kijamii katika moja ya wilaya nchini na haijafahamika atapangiwa wilaya gani kutekeleza adhabu yake hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...