Mzunguko wa Tano wa Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi “CDF Cup 2018” yanatarajiwa kufungwa rasmi leo tarehe 18 Mei, 2018 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa kuzikutanisha timu za mpira wa miguu ya Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi na Kamandi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). 
Mashindano hayo yalifunguliwa rasmi tarehe 08 Mei 18 huku yakishirikisha Kamandi zote za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambazo ni Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi, Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu, Kamandi ya Jeshi la Anga, Kamandi ya Jeshi la Wanamaji na Kamandi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). 
Timu hizo zimechuana vikali katika michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete, Mpira wa Kikapu, Mpira wa Wavu, Mpira wa Mikono, Ngumi za Ridhaa, Riadha na Ulengaji Shabaha. 
 Kamandi zote zimefanya vizuri lakini Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi na JKT zimeonesha ushindani mkubwa katika michezo mbalimbali hadi kufika hatua za fainali. 
Mpaka sasa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi imeonesha kushinda michezo mingi zaidi ikilinganishwa na Timu zingine.
Mchezaji wa timu ya Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi akirusha mpira dhidi ya Kamandi ya Jeshi la Kujenga Taifa katika mchezo wao Uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam. Picha na JWTZ

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...