Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amewataka wananchi wa wilaya ya Mkalama iliyopo mkoani Singida kushikamana ili kuinua wilaya yao kimaendeleo.


Waziri Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa akihutubia umati wa wananchi wa wilayani hiyo katika shughuli za uzinduzi wa wiki ya elimu inayofanyika wilayani Mkalama.Jafo amebainisha kwamba wilaya ya Mkalama ilikuwa wilaya ya mwisho katika matokea ya darasa la saba ya mwaka 2017 hivyo wanapaswa kushikamana kuondoa aibu hiyo.



Katika mkutano huo, amempongeza Mbunge wa Jimbo hilo kwa kazi kubwa anayofanya ambayo imesaidia kusukuma maendeleo wilayani humo kwa kushirikiana vyema na serikali na kufanikisha miradi ya afya, maji, pamoja na elimu. Aidha amesema kwasasa serikali inaboresha kituo kimoja cha afya na pia anefanikisha  mpango kabambe wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ambayo imepangwa kujengwa katika bajeti ya 2018/2019.



Kadhalika, Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkalama kumwita mkandarasi aliyejenga jengo la halmashauri ambaye ni Kampuni ya Mzinga kurudi haraka ndani ya wiki ijayo ili arekebishe maeneo yenye dosari.Pamoja na hayo, Jafo amesisitiza watumishi wote kuwa waadilifu kwani Ofisi yake anayoiongoza haiwezi kuvumilia ufisadi, wizi, uzembe, na ubabaishaji kazini.


Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akisalimiana na viongozi na wananchi wa wilaya ya Mkalama.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Rehema Nchimbi akimtembeza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kwenye vikundi mbalimbali vya burudani.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Rehema Nchimbi akimkaribisha Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kuzungumza katika uzinduzi wa wiki ya elimu.
Jengo la Halmashauri ya Mkalama ambalo Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo ameagiza lifanyiwe marekebisho.
Baadhi ya vikundi vya burudani vikitumbuiza katika uzinduzi wa wiki ya elimu wilayani Mkalama

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...