Na John Nditi, Morogoro
MKUU wa Mkoa Morogoro  Dk  Kebwe Stephen  Kebwe amezindua bodi ya parole na kuvitaka vyombo vinavyoshughulikia HAKIJINAI kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwa Jeshi la Magereza ili wafungwa wote wanaostahili kunufaika na mpango huo, wanufaike bila kucheleweshwa.
Dk Kebwe alisema hayo katika kwenye kikao cha uzinduzi wa Bodi hiyo kwenye uumbi wa  Magereza Club uliopo kwenye uwanja wa Mwalimu Nyerera wa Nane Nane , mjini Morogoro. Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wajumbe wote  kutoa ushirikiano wa karibu na Katibu wa Bodi ya Parole Mkoa wa Morogoro ilikufanikisha malengo na makusudi yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria.
Naye Katibu wa Bodi ya Parole Mkoa wa Morogoro Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Magereza , Mzee Ramadhani Nyamka ambaye pia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro alieleza kuwa bodi hiyo  ilianzishwa na sheria ya Bodi ya Parole namba 25/1994 na GN. No.563/199. Pia alitaja kuwa , kanuni za Bodi ya Parole zilitangazwa n a kuchapishwa katika gazeti la serikali GN. No. 783/1997  Desemba 26, 1997 .
Hata hivyo alisema  Bodi ya Parole inakabiliwa na changamoto katika utekelezaji wa sheria hiyo na hizo ni pamoja na ugumu wa upatikanaji wa nakala za hukumu kwa wakati kutoka katika mahakama zilizowafunga, taarifa za uhalifu kutoka katika vituo vya Polisi vilivyo wakamata na upatikanaji wa maoni ya waathirika wa matukio.
Nyamka alisema,  mpaka sasa Bodi ya Parole Taifa imeachilia jumla ya wafungwa  177  kutoka katika Magereza Mkoa wa Morogoro, kati ya hao wafungwa 157 wa mekwishamaliza vifungo vyao na wafungwa 20 waliosalia wanaendelea kutumikia adhabu zao katika jamii. 
Katika kikao hicho,  Bodi hiyo  ilifanya uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa Bodi wa Parole chini ya usimamizi wa Mwenyekiti mteule James   Celestine ambapo wajumbe wa limpendekeza , Wariambora Nkya kuwa makamu mwenyekiti baada ya kukidhi sifa na vigezo vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria na kukubaliwa na wajumbe wa Bodi ya Parole. Baada ya uchaguzi huo, wajumbe walijadili na kupendekeza majalada ya wafungwa saba wenye sifa ya kunufaika na mpango huo wa Parole.
 MKUU wa Mkoa Morogoro  Dk  Kebwe Stephen  Kebwe  ( kati kati walioketi) akiwa na wajumbe wa bodi ya parole mkoa wa Morogoro baada ya kuizidua. Kulia ni Katibu wa Bodi ya Parole Mkoa wa Morogoro Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Magereza , Mzee Ramadhani Nyamka ambaye pia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro
 Mkuu  wa Mkoa Morogoro  Dk  Kebwe Stephen  Kebwe ( aliyesimama) akizungumza jambo kabla ya kuzindua rasmi  bodi ya parole mkoa wa Morogoro.
Mkuu  wa Mkoa Morogoro  Dk  Kebwe Stephen  Kebwe akiwa katika picha na wajumbe wa  bodi ya parole wa mkoa huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...