Serikali imejipanga kuwajengea Kisima cha kisasa watu wenye mahitaji maalum kitachoweza kuhudumia Kaya 26 zenye jumla ya watu 56 wenye ukoma na wazee katika Kambi ya Samaria Hombolo jijini Dodoma.

Hatua hiyo inakuja mara baada ya wakazi wa kambi ya Samaria kueleza changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo; ukosefu wa maji salama, changamoto za matibabu kwa kukosa bima za afya, uchakavu wa  magodo kwa ajili ya malazi, uhaba wa chakula cha uhakika.

Changamoto hizo zimeibuliwa wakati ya Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa alipoambatana na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso Mei 23, 2018 katika Makazi ya watu wenye mahitaji maalum ikiwemo wazee na watu wenye ukoma.

“Watu wenye mahitaji maalum ikiwemo wenye ukoma wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya maji eneo la Samaria, sisi kama Serikali tumedhamiria kuwajengea kisima cha kisasa kitakachotoa maji baridi na kuweza kuhudumia makambi haya pamoja na kijiji chote cha Samaria”.alisema Naibu Waziri Ikupa

Naye Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ameiagiza timu ya waataalamu kutoka Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa kuanza kazi hiyo mara moja.

“ Naagiza timu ya wataalamu kuja kupima maeneo ambayo yatafaa kwa ajili ya uchimbaji wa kisima hicho” .alisema Aweso
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa akizungumza jambo na wakazi wa Kambi la wenye Ukoma la Samaria lilipo Kata ya Hombolo Bwawani mkoni Dodoma alipowatemnbelea kutatua changamoto wanazokabiliana nazo tarehe 23 Mei, 2018, kulia kwake ni Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe Jumaa Aweso.
 Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe Jumaa Aweso akiwahakikishia wakazi wa Samaria utatuzi wa changamoto ya maji inayowakabili kwa kuahidi kuanza uchimbaji  wa kisima cha maji baridi baada ya kufanya ziara alipoambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa Mei 23, 2018.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa akiwasiliza baadhi ya wakazi wa Kambi la wenye Ukoma la Samaria alipowatembelea Mei 23, 2018 kwa kutatua changamoto ya maji kwa kuahidi kuanza ujenzi wa Kisima cha maji baridi Kijijini hapo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa na Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji (katikati) pamoja na Meneja Kanda ya Kaji kutoka Wakala wa Uchimbaji wa Visima na mabwawa, Khalifu Utali wakiwasililiza wakazi wa Makazi ya wenye ukoma walipowatembelea Mei 23, 2018.
 Diwani wa Kata ya Hombolo Bwawani, Mathayo Ndahilo akitoa maelezo mafupi kuhusu Kituo cha Watu wenye mahitaji maalum cha Samaria wakati wa Ziara ya Manaibu waziri Mhe Stella Ikupa (Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu) na Jumaa Aweso (Wizara ya Maji na Umwagiliaji) walipotembelea Makazi hayo Mei 23, 2018.
 Baadhi ya watu wenye ukoma wanaoishi katika makazi ya Samaria wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa (hayupo pichani) wakati alipowatembelea kutatua baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kambini hapo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...