Na Mwandishi wetu
TAASISI ya Dr Ntuyabaliwe imezindua shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni wenye lengo la kuibua vipaji vya watoto katika kubuni na kutunga hadithi.
Shindano hilo linatarajiwa katika siku za usoni kufika Tanzania nzima.
Uzinduzi huo umefanywa katika shule ya msingi Kinondoni wilayani Kinondoni.
Akizindua shindano hilo Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya alisema shindano hilo ni muhimu kwa nchi hii hasa katika kukuza uwezo wa kusoma na kuandika na kuibua vipaji vya wanafunzi katika kukuza lugha ya Kiswahili na ubunifu.
Alisema kwamba serikali inafurahishwa na jinsi taasisi hiyo inavyofanywa ya kuibua vipaji vya watoto na kukuza lugha ya Kiswahili kwa kuangalia usomaji wa vitabu na shindano la andika challenge.
Alisema anajua kwamba Taasisi hiyo ilianza na maktaba katika shule za msingi na kuhamasisha usomaji wa vitabu na sasa wanakuja na shindano hilo litakalosambaa nchi nzima.
Alisema andika challenge ni muhimu kwa watoto.
“Tunaamini kuwa tunaenda kukuza vipaji vya watoto…katika kutunga hadithi kwa kuongoza watoto katika kuhakikisha kwamba uchaguzi wa mada zinakuwa na maana zikizingatia fani na maudhui, moja ya tanzu au kipera cha simulizi “ alisema.
Mwalimu
Mkuu wa shule ya msingi Kinondoni, Bw Emmanuel Ntenga akizungumza
machache na kuitambulisha meza kuu wakati wa hafla ya uzinduzi wa
shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya
Kinondoni iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es
Salaam. Kutoka kushoto ni Mtendaji wa Kata ya Mwananyamala, Mickidadi
Ngatumbura, Mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther
Kaaya, Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi
pamoja na Afisa Elimu kata ya Mwananyamala, Joshua Biswalo wakiwa meza
kuu.
Mgeni
rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya akizungumza
na wanafunzi pamoja na walimu wa shule ya msingi Kinondoni wakati wa
hafla ya uzinduzi wa shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za
msingi manispaa ya Kinondoni iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni
hapo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr
Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi pamoja na Mtendaji wa Kata ya
Mwananyamala, Mickidadi Ngatumbura (kushoto).
Mgeni
rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya akitoa
mkono wa pongezi kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi.
Jacqueline Mengi wakati wa hafla ya uzinduzi wa shindano la Andika
Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni
iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza kuhusu
vigezo vya kushiriki na zawadi kwa tano bora kwa wanafunzi wa shule za
msingi manispaa ya Kinondoni watakaoshiriki shindano la Andika
Challengekatika hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika kwenye ukumbi wa
maktaba ya shule ya msingi Kinondoni mwishoni mwa wiki jijini Dar es
Salaam.
Mwanafunzi
Brian Jackson wa darasa la saba shule ya msingi Kinondoni akitoa neno
loa shukrani kwa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe kwa kuzindua shindano hilo
la andika challenge wakati hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa
maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Mwanafunzi Blessing Elianoki wa darasa la sita.
Mgeni
rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya pamoja na
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi wakizundua
shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya
Kinondoni katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba
shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Sehemu
ya waandishi wa habari na baadhi ya walimu wa shule ya msingi Kinondoni
waliohudhuria uzinduzi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa
shule za msingi manispaa ya Kinondoni katika hafla fupi iliyofanyika
kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es
Salaam.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya msingi Kinondoni waliowakilisha wenzao katika
hafla fupi ya uzinduzi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa
shule za msingi manispaa ya Kinondoni iliyofanyika kwenye ukumbi wa
maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi katika picha ya
pamoja na baadhi ya walimu wa shule ya msingi Kinondoni mara baada ya
kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa shindano la andika challenge kwa
watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni uliofanyika kwenye
ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi katika picha ya
pamoja na baadhi ya wanafunzi na baadhi ya walimu wa shule ya msingi
Kinondoni mara baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa shindano la
andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni
uliofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi katika picha ya
pamoja na mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther
Kaaya, Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kinondoni, Bw Emmanuel Ntenga
pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo waliowakilisha wenzao katika
hafla fupi ya uzinduzi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa
shule za msingi manispaa ya Kinondoni uliofanyika kwenye ukumbi wa
maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...