*Yatoa shukrani kwa Rais Magufuli kufuatilia ujenzi wa msikiti mkuu Bakwata

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

BARAZA Kuu la Waislam Tanzania(BAKWATA)limetoa maelekezo ya kuutangaza mwandamo wa Ramadhan huku likifafanua kuna kamati maalum inayoongozwa Mufti wa Tanzania Aboubakar Zuber ndio itakayotangaza mwandamo huo baada ya kuthibitika kuonekana.

Akizungumza leo Dar es Salaam Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata na Msemaji wa Mufti wa Tanzania Sheikh Hamis Mataka amesema kuwa mwandamo wa mwezi unatarajiwa kutangazwa kesho kwa utaratibu maalumu uliowekwa na baraza hilo.
Amefafanua kote duniani kumekuwa na utaratibu wa kuufuatilia mwandamo wa mwezi na kisha kuutangaza na hivyo utaratibu pia unafanywa na Bakwata kupitia kamati maalum ya kufuatilia mwandamo.
"Zanzibar wanacho chombo cha kufuatilia mwanandamo wa mwezi na kuutangaza, pia Kenya wanachombo cha kutangaza. Kwa Tanzania Bara kuna kamati maalum ya kufuatilia na kuutangaza mwezi na kamati hiyo inaongoza na Mufti wa Tanzania,"amesema.
Amesema kesho Alhamis ndio tarehe 29 ya Ramadhan na magharibi yake mwezi utafuatiliwa kama umeandama na kisha kuuutangaza. Amefafanua pamoja na kuwepo kwa kamati ya kufuatilia mwandamo bado umma nao unayo nafasi ya kuufuatilia na kisha watatoa taarifa kupitia utaratibu uliopo.
"Bahati nzuri Bakwata ina mtandao mkubwa kote nchini kuanzia msikiti, hivyo kinachotakiwa ni kutoa taarifa kwa imamu ya msikiti,"amesema.Ameongeza mwezi haundami chumbani bali ni hadharani, hivyo anayeuona anatoe taarifa kwa imamu wa msikiti ambaye naye baada ya kuuthibitisha atatoa taarifa makao makuu Bakwata na kisha kuutangaza rasmi.

MUFTI AMSHUKURU RAIS MAGUFULI
Wakati huo huo Sheikh Mataka amesema Mufti wa Tanzania anatoa shukrani kwa Rais Dk.John Magufuli kutokana na jitihada zake za kuufuatilia ujenzi wa msikiti mkubwa unaojengwa katika eneo la Bakwata.

"Jana Rais alifanya ziara ya kuja kuangalia ujenzi wa msikiti unaoendelea kujengwa .Baada ya kukagua ujenzi alitoa mchango wa Sh.milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa msikiti huu unaojengwa na Mfalme wa Moroco.

"Tunafahamu hata ujenzi huu kuanza kwake umetokana na jitihada za Rais ambaye alitoa ombi kwa mfalme Mohamed wa VI ambaye alikubali kujenga msikiti huo ambao utakuwa mkubwa.Pia kutakuwa na kumbi za mikutano na vitega uchumi.Mufti wa Tanzania kwa niaba ya Bakwata na Waislamu nchini anatoa shukrani nyingi kwa Rais,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...