Jumamosi tarehe 23 Juni, 2018 Mhe. Asha-Rose Migiro, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za uzinduzi wa Jumuiya Mwamvuli ya Watanzania waishio nchini Uingereza na Ireland ya Kaskazini iitwayo ATUKAssociation of Tanzanians in the UK.
Jumuiya hii inatokana na muungano wa jumuiya za Diaspora kutoka mikoa mbalimbali ya Uingereza na wanachama wa kujitegemea.
Wajumbe wa Kamati ya Muda iliyoratibu kuanzishwa kwa ATUK walipongeza na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za kupambana na ufisadi, kusimamia uwazi na uwajibikaji katika utumishi wa umma na kuongeza kasi ya kujenga uchumi wa viwanda. Kauli mbiu ya hafla hii ilikuwa “UMOJA NI NGUVU, TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA”. Hivyo mojawapo ya malengo ya kuanzishwa kwa ATUK ni kujenga umoja na kukusanya nguvu za kuchangia jitihada za kujenga uchumi wa viwanda nchini mwetu.
Akihutubia hadhara hiyo Balozi Migiro aliwapongeza ATUK na alihimiza umoja na kukumbusha kwamba wakati wote Mhe. Rais amekuwa akisisitiza umoja wa Watanzania bila kujali tofauti zao kwani umoja ni nyenzo muhimu ya kujiteletea maendeleo.
Hivyo Balozi Migiro aliwashukuru kwa Muungano huo na kueleza kwamba wakiendeleza mshikamano wataweza kuchangia  kwa ufanisi jitihada kubwa za Mhe. Rais Magufuli na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwaletea maendeleo Watanzania wote.
 Mhe Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza na Ireland ya Kaskazini Dr Asha Rose Migiro akikata cake katika uzinduzi wa Jumuiya Kuu ya Watanzania Uingereza sherehe hizo zilizofanyika mjini Reading na kuhudhuriwa na mamia ya Watanzania pamoja na wawekezaji wenye nia ya kuwekeza Tanzania nchi iliojaliwa amani na utulivu katika Africa. Kutoka kushoto ni Joe Warioba Kamati Maalum, katikkati Mhe Balozi Asha Rose Migiro, Dr Donald Mlewa, na Bi Neema Kitilya Kamati Maalum. Lengo la Jumuiya na Kauli mbiu ya Watanzania wa Uingereza ni "Umoja ni Nguvu na Tanzania ya Viwanda inawezekana".

Sehemu ya Watanzania wakiwa  kwenye sherehe za uzinduzi wa Jumuiya Mwamvuli ya Watanzania waishio nchini Uingereza na Ireland ya Kaskazini iitwayo ATUKAssociation of Tanzanians in the UK mjini Reading Jumamosi
 Watoto wakitumbuiza kwa wimbo maalumu
 Sehemu ya waliohudhuria sherehe hizo
 Wanajumuiya wakiwa kwenye sherehe hizo
Ukumbi ulijaa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. I was just wondering, huyu balozi kaletwa kutugawa au kututenganisha? How can she come to this function? Anajua (she has to know)kwamba kuna jumuia nyingine ya wa TZUK diaspora yet kaaamua kuitambua jumuia hii mpya ambayo so far haijaonyesha viongozi wake....This is contradiction. President magufuli huyu mama balozi atatugawa. She was suppose to call all the leaders of all known jumuia, sit down with them and come up with one jumuia so that we can move on from there. Is it politics?
    I am just saying..

    ReplyDelete
  2. Yaaani wewe ndio unayetaka kuwagawanya watanzania. Maneno unayosema si kweli kabisa. Kiongozi wenu na Makamu wake waliitwa kwenye mukatano na walihudhuria. Badaye officially kwa email alisema kwamba TZUK diaspora haitashiriki. Uthibitisho upo. Nyinyi ndio hampendi maendeleo ya watanzania. Kazi yenu ni kutukana na kukashifu watu. Nyinyi ndio wabinafsi na kula hela za wanachama.
    Mulizeni kiongozi wenu pesa za watu kazifanya nini mpaka anataka kushtakiwa. Watanzania Uk sio wajinga wamesha washtukia.
    Hongera sana Mama Balozi Na Kamati ya ATUK. A job well done����������������

    ReplyDelete
  3. Hongera Mheshimiwa Balozi wetu wa nchi ya watanzania hapa UK, kipenzi mama Dr Asha Rose Migiro
    ----------------------------------------------------------------------------------------------

    Hakika tunakushukuru sana Rais wetu kipenzi Dr John PomBe Magufuli kwa kututeulia mama huyu Dr Asha kwani anafanya kazi kubwa sana ya kutuunganisha sisi wa Tanzania wazelendo wa nchi yetu. Serikali ya awamu ya Tano sera kuu yake ni Tanzania ya viwanda inawezekana kwa falsa ya " Hapa Kazi tu". Sisi watanzania tuliopo nje ya nchi tunayofuraha kuunda Jumuiya ATUK inayo itambua serikali yako Mh Magufuli na Juhudi zako na kwa hapa kupitia mwakilishi wako mama Dr Asha Rose Migiro... tutajitahidi kuhamasisha uwekezaji mdogo na mkubwa kwetu nyumbani Tanzania. Miongoni mwetu tuna wanajumuiya wengi wasomi wakiwemo madaktar, ma enginieer, wanasheria nk. Pamoja ya hayo sisi wan ATUK tukishirikiana na ubalozi wetu pia dhamira yetu pamoja ya kusaidiana wenyewe kwa wenyewe, tunayo nia kwa vitendo kuhakikisha tunasaidia maendeleo ya kijamii kwawatanzania wenzetu walipo Tanzania. Tunaipenda nchi yetu tuna mpenda Balozi wetu tunakupenda Rais wetu JPM, kwa pamoja tutashinda baba. Asante mama Asha Rose Migiro kwa kutuunganisha.

    Hao wanojiita TZUK, sina la kusema zaidi ya kujiuliza swali, kuna mtoto anazaliwa bila mzazi? na je, mtoto anaanzaje kumkataa baba yake na mama yake mzazi huku akimtegemea ada, malezi na matunzo kwa ujumla. Unajiita mtanzania, nchi mama ni Tanzania, Serikali iliyopo madarakani inasimamia Tanzania. Unapoaanza kuukana na kutupia mawe ubalozi ambao ndio mwakilishi wa nchi yetu na serikali yetu hasa mh Rais, je, hapoutakuwa na uzalendo upi wakujiita mtanzania?


    Alipokua waziri mkuu, aliagiza, tuvunje vikundi vidogovidio tuanze upya kuunda Jumuiya ya Pamoja nchi ya weledi elekezi kutoka ubalozi wetu, wala hakuona iko haja ya kuchanganya maswala ya utofauti wa itikandi za vyama na makabila…. Iweje leo tupinngane na Maoni ya baba yetu mh waziri mkuu Kassim Majaliwa?



    ushauri

    1. vema tukaangalia wapo tume teleza, tukasababisha uwepo wa ATUK NA TZUK?

    2. HATA iwe vipi: unawezaje kujitenga na mwakilishi wa serikali ya nchi yako UK, yet ukiwa na shida unaenda ubalozini na unataka serikali ikutambue?


    penye zuri nene, penye baya ndio urimbo


    Jun 25, 2018

    ReplyDelete
  4. Hassan Khalfani umeuliza swali zuri kaka, why ATUK na TZUK? This was exactly my point. Nilitegemea mama balozi angefind out why? kama kuna tofauti ya katiba kati ya makundi haya mawili ndo angewaweka chini na kuzungumza nao (kama hao ATUK wana katiba). Kama haya yote yameshafanyika we need to know. ATUK na TZUK msitugawe na msitugombanishe na balozi wetu. Whatever the difference we can resolve this democratically kama tulivyochaguana vivyo hivyo tunaweza kufanya mabadiliko. There r too many Tanzanians behind TZUK and ATUK. Acheni siasa. ATUK u r as bad as TZUK if u will not merge these two jumuia.
    I am just saying...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...