Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Exim Tanzania, Bw Jaffari Matundu akipeana mkono na Marleen Jansen, Afisa Mkuu wa Uwekezaji, wa benki ya Maendeleo ya Uholanzi – FMO baada ya kusaini mkataba wa mkopo wa shilingi bilioni 75 ili kuwekeza kwenye mfuko wa mikopo ya muda mrefu wa biashara ndogo ndogo na za kati (SME) nchini Tanzania.

BENKI ya Exim Tanzania imetangaza kuchukua mkopo wa kiasi cha shilingi bilioni 75 kutoka kwa benki ya Maendeleo ya Uholanzi – FMO, ili kuwekeza kwenye mfuko wa mikopo ya muda mrefu wa biashara ndogo ndogo na za kati (SME) hapa nchini 

Benki imechukua mkopo huo ili kuziba pengo kubwa la mikopo kwa biashara ndogo ndogo na za kati nchini ambazo zinakadiriwa kuwa ni takribani kampuni milioni 3. Vilevile utafiti unaonyesha kuwa idadi kubwa ya kampuni hizi (zinazoajiri watu chini ya watano) zinamilikiwa na familia na zinapatikana hasa katika miji midogo na maeneo ya vijijini.

Ingawa takwimu za kiutafiti kwenye biashara ndogondogo na za kati sio za kutosha, data zilizopo zinaashiria kuwa SME ni sekta yenye umuhimu mkubwa katika uchuni. Kampuni hizi nyingi huwa hazina nafasi ya kupata huduma za kifedha ingawa kuna asilimia ndogo ambayo inategemea huduma za kifedha kutoka kwenye taasisi zisizo za kifedha kama vile kupitia mitandao ya simu ambapo huduma za kutuma fedha ni gharama kubwa. 

Akizungumzia hatua hiyo ya benki ya Exim, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Jaffari Matundu alisema "Hatua hii ni samabamba na dira ya Mheshimiwa, Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ya kutaka kubadilisha Tanzania kuwa ya nchi inayotegemea uchumi wa viwanda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...