Ulinzi wa Faru katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti na maeneo ya jirani, unatarajiwa kuimarika zaidi baada ya kuanza mradi maalum wa Faru kufungwa vifaa vya technolojia za kisasa na hivyo kuwalinda na matishio ya ujangili ama kupotea.

Faru ni miongoni mwa wanyama ambao wapo hatarini, kutoweka duniani, kutokana na kuwindwa na majangili, ambao wamekuwa wakiuza pembe zao na hivyo serikali imekuwa na mikakati kadhaa ya kuimarisha ulinzi wao.

Akizungumza na wanahabari, Mwakilishi mkazi wa shirika la uhifadhi la kimataifa la Frankfurt zoological Society moja ya mashirika yanayoratibu mradi huo, Gerald Bigulube alisema mradi huo wa aina yake barani Afrika, unatarajiwa kuimalisha ulinzi na ufatiliaji wa faru katika eneo la Seregeti.

Alisema mradi huo unatarajiwa kutumia zaidi ya sh 253 milioni, zilizotolewa na shirika la uhifadhi la Friedkin Conservation Fund(FCF) na unaratibiwa pia na Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA) na Taasisi ya utafiti wa Wanyamapori(TAWIRI). Bigulube alisema, tayari utekelezaji wa mradi huo, umeanza, ambapo mwaka jana faru 21 walifungwa vifaa maalum digital VHF na mwaka huu wengine watafungwa vifaa vya kisasa zaidi kutumia mfumo wa LoRa(LoRa System).

"lengo letu kama wahifadhi ni kuhakikisha Faru waliopo nchini wanaongezeka zaidi sambamba na wanyama wengine ambao maisha yao yamekuwa hatarini wakiwepo Tembo ambao nao tayari kuna miradi ya kuwafunga vifaa vya kisasa ili kuwafatilia "alisema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...