Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, jalada halisi la kesi inayowakabili vigogo wawili wa uthamini wa madini ya almasi wa Serikali lipo kwa Mkurugenzi wa mashtaka ( DPP).

Wakili wa Serikali Esterzia Wilson ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipokuja mahakamani hapo kwa kutajwa.Amedai kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika na jalada halisi lipo kwa DPP, hivyo akaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Kutokana na taarifa hiyo, Hakimu Mashauri aliiahirisha kesi hiyo hadi Juni 18 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mkurugenzi wa Uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania (Tansort) Archard Kalugendo na mthamini almasi wa serikali, Edward Rweyemamu ambao ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na Madini.

Wote wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wakidaiwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh.bilioni 2.4. Kalugendo na Rweyemamu wanasota rumande kutokana na DPP kuzuia dhamana zao.Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa wanakabilkiwa na ashtaka la kuisababishia serikali hasara ya Sh. 2,486,397,982.54 ambapo wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Agosti 25 na 31, mwaka 2017 katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Shinyanga.

Washtakiwa hao wanadaiwa kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathaminishaji wa almasi wa Serikali na waajiriwa wa wizara hiyo waliisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani 1,118,291.43 ambazo ni sawa na Sh.2,486,397,9.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...