Na Shushu Joel, Simiyu

NAIBU waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ametoa wito kwa Halamshauri zote nchini kubuni miradi ya kimkakati ya itakayoziongezea mapato badala ya kuendelea kutegemea ushuru na tozo mbalimbali kutoka kwa wananchi.

Dkt. Kijaji alisema hayo wakati alipotembelea kiwanda cha kutengeneza chaki cha wilaya ya Maswa wakati wa ziara yake ya kujionea utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Vwanda Mkoani Simiyu akiwa na viongozi wa Halmashauri na Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kondoa.

Aliongeza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Halmashauri zote zinabuni miradi ya kimkakati ambayo itaziongezea mapato na akatoa wito kwa Halmashauri zote nchini kujifunza kwa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ambayo imetengewa shilingi bilioni 8.2 na Serikali kwa ajili ya kutekeleza miradi miwili ya upanuzi wa Kiwanda cha Chaki na kujenga kiwanda cha vifungashio.

“Niwapongeze Simiyu mnafanya kazi nzuri, tunataka kuondoka kwenye ule ukawaida wa Halmashauri zetu kulalamika kuwa Serikali Kuu imechukua vyanzo vya mapato, Serikali Kuu haijachukua kinachohitajika ni ubunifu wa miradi kama Halmashauri ya Maswa ilivyofanya, nitoe wito kwa Halmashaui zote kubuni miradi, Serikali ipo tayari kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya kimkakati ya kuongeza mapato ya Halmashauri” alisema

Naye mbunge wa Maswa Mashariki na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ameiomba Serikali kutoa fedha hizo shilingi Bilioni 8.2 zilizotengwa kwa wakati ili Miradi iliyokusudiwa ya upanuzi wa kiwanda cha chaki na ujenzi wa kiwanda cha vifungashio iweze kutekelezwa kwa wakati.

Kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Dkt. Fredrick Sagamiko alisema Halmashauri hiyo imedhamiria kufikisha zaidi ya asilimia 75 ya mapato ya ndani yatakayotokana na viwanda vilivyopo na vinavyoendelea kujengwa wilayani humo ili kuondokana na kutegemea fedha za miradi kutoka serikali kuu.

Aliongeza kuwa katika kukiongezea kiwanda cha chaki uwezo wa uzalishaji, Halmashauri ya Maswa imenunua eneo kwa ajili ya malighafi ya kutengenezea chaki katika Mkoa wa Singida.Awali Dkt. Ashatu alitembelea eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya uwekezaji katika viwanda la Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mahali ambapo patajengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza chak(upanuzi wa hiki kilichopo) na kujenga kiwanda cha vifungashio.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akikabidhiwa boksi la chaki za Maswa (Maswa Chalks) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka baada ya kutembelea kiwanda cha Chaki wilayani Maswa akiwa na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na CCM wilaya ya Kondoa kwa lengo la kujifunza utekelezaji wa sera ya viwanda mkoani humo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alipotembelea kiwanda cha Chaki wilayani Maswa mkoani Simiyu ambapo aliongozana na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na CCM wilaya ya Kondoa kwa lengo la kujifunza utekelezaji wa sera ya viwanda mkoani humo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akiangalia viatu vya ngozi vinavyotengenezwa katika kiwanda cha Senani wilayani Maswa mkoani Simiyu baada ya kutembelea kiwanda cha Chaki wilayani Maswa akiwa na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na CCM wilaya ya Kondoa kwa lengo la kujifunza utekelezaji wa sera ya viwanda.(PICHA ZOTE NA SHUSHU JOEL).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...