Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wasafirishaji wa Mabasi Tanzania(TABOA) Enea Mrutu amewaomba wamiliki wote wa mabasi nchini kuendelea kutoa huduma za kusafirisha abiria kwa umakini wa hali ya juu kwa kuhakikisha hawasababishi ajali wakati wakiendelea kusubiri kukuona na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ili watoe kilio chao.

TABOA iliomba kuonana na Waziri Mkuu kwa ajili ya kutoa malalamiko yao kutokana kwa madai kuna sheria na kanuni za usalama barabarani ambazo  ni kandamizi kwao na zimekuwa zikiwaweka katika wakati mgumu katika kutoa huduma ya kusafirisha abiria nchii.

Hata hivyo TABOA bado hawajafanikiwa kuonana naye ingawa tayari ameshawapa maelekezo kuwa wakati wowote atakutana nao na kisha kuwasikiliza ili kupata muafaka kwa kushirikiana na wadau wengine wa usafiri wakiwamo Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).

Akizungumza na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam Mrutu amesema wanatambua majukumu aliyonayo Waziri Mkuu hivyo wana imani akipata muda watakutana naye na kisha kuzungumza kwa kina kuhusu changamoto ambazo wanakabiliana nazo watoa huduma ya usafiri nchini.

"Ombi letu kwa wanachama wa Taboa waendelee kutoa huduma bora ikiwa pamoja na kuwa makini barabarani ili kuepuka ajali.Tunamatumaini makubwa na Waziri Mkuu, hivyo tunajua akipata muda atatuita ,nasi tupo tunasubiri.Hivyo wakati tunaendelea kumsubiri tuendelee kutoa huduma ya usafiri bila kuchoka,"amesema Mrutu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...