Pamoja ya kuwa kampuni inayosifika katika uzalishaji wa simu zinazotunza chaji, kampuni ya simu ya TECNO imeendelea kudhihirisha ubora wake kwa mara nyengine tena kupitia TECNO pouvoir 2 (TECNO LA7) ikiwa ni muendelezo wa ‘TECNO L series’ yenye betri 5000mAh na mtandao wa 4G.
Na pamoja ya kuwa na betri kubwa aina ya Li-Polymer, 5V2A yenye kujaa chaji kwa haraka na kudumu nayo zaidi ya siku tatu lakini bado kampuni ya simu ya TECNO hakusita kuhakikisha TECNO pouvoir 2 inakuwa na muonekano mzuri kwa kupitia umbo lake jembamba la ‘metallic’ lenye kutawaliwa na wigo mpana wa kioo chenye uwiano wa 18:9.
TECNO pouvoir imebeba kamera mbili nyuma ikiwa na megapixel 13 na flashi mbili za LED na mbele ikiwa na megapixel 8 na LED flashi pamoja na mix flashi zenye kupiga picha nzuri na zenye wang’avu kutokana  na aina ya kioo cha TECNO pouvoir 2 kuwa na upana wa nchi 6.0 HD+ (1440*720) 450nit IPS. Mix flashi inafanya kazi kama ilivyo kwa flashi za kawaida isipokua yenyewe inapatikana ndani ya kioo cha simu na inafanya kazi wakati wa kupiga ‘selfie’ tu.
Na ikiwa simu ya kwanza kwa toleo la ‘TECNO L series’ kuwa na kasi ya mtandao wa 4G lakini pia TECNO pouvoir 2 inaufanisi mzuri zaidi kutokana na processor ya MT6739WA 1.3 ghz Quard-core pamoja na Android 8.1 Oreo na HiOS ya 3.3.

TECNO pouvoir 2 inatumia aina tofauti tofauti za ‘security’ ikiwamo fingerprint inayopatikana nyuma ya simu na face id yenye kunlock simu kupitia paji la uso na ndio simu ya kwanza ya toleo la ‘TECNO L series’ kutumia face id.
Simu hii pia imekuja na memory ya ndani ya GB 16 na GB 2 za ram vinavyoiwezesha simu kuhifadhi mafile mengi na kufanya kazi zaidi ya moja kwa wakati mmoja pasipo kuathiri uwezo wa simu lakini pia TECNO pouvoir inaweza kubeba hadi GB 64 memory ya ziada.
TECNO pouvoir 2 inapatikana katika rangi tatu tofauti nyeusi, gold na city blue.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...