Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

CHUO Cha Kodi (ITA)kimeanzisha klabu mpya katika shule za sekondari na vyuo ili kuanza kuwajenga na kuwaandaa  wanafunzi kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu kodi na umuhimu wake kwa Taifa.

Akizungumza katika Maonyesho ya 13 ya Vyuo Vikuu ya Elimu ya Juu Tanzania (TCU)yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Ofisa Udahili wa ITA Pascal Gomba amesema kila mwanannchi anahitajika kujua elimu ya kodi ili awe analipa kodi kwa wakati.

"Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)iliamua kuanzisha klabu za wanafunzi mashuleni kwa ajili ya kueneza elimu kwa watu wengi zaidi.Tunaamini utararibu huu utaongeza chachu ya wananchi kulipa kodi kwa maslahi ya Taifa letu,"amesema.Gomba amefafanua klabu hizo zimeanzia kwa shule za sekondari zilizopo Mkoa wa Dar es Salaam na ametaja baadhi ya shule hizo ni Jangwani,Zanaki,Kibasila,Kisutu,Loyora na Makongo.

"Kujiunga katika klabu za kodi ni moja ya mikakati ya TRA kuhakikisha elimu ya kodi inafahamika kwa kila mwananchi kuanzia ngazi ya wanafunzi hadi watu wazima,"ameongeza  Gomba.Wakati huo huo amesema uchumi wa Tanzania unakuwa kwa sababu ya ukusanyaji mzuri wa kodi na wananchi wenyewe kujituma kulipa kodi kwa hiari.

Hata hivyo Gomba amewataka wanafunzi kujiunga katika chuo cha ITA kwani  Serikali inahitaji zaidi wataalamu wa ukusanyaji wa kodi kwa manufaa ya taifa.Kuhusu uwepo wao kwenye maonesho hayo, Gomba amesema lengo kuu ni kuwaonesha wanafunzi na wananchi kwa ujumla kozi zinazotolewa katika chuo chao.

Amesema taasisi za Serikali na za binafsi zinahitaji mtu mwenye ujuzi wa ukusanyaji wa kodi kwa ajili ya kufanya shughuli zao za uzalishaji.

"Kuna umuhimu mkubwa kwa vijana wa Tanzania na hata wale watu wazima kujiunga katika Chuo cha Kodi,"amesema na kuongeza kwa sasa wanaendelea kupokea wanafunzi kwa ajili ya mwaka wa masomo wa 2018.

Moja ya maofisa wa chuo cha kodi akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...