Na Shani Amanzi
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba
amewataka waandikishaji waliopata Mafunzo ya maboresho ya Mfuko wa Afya
ya Jamii (CHF Iliyoboreshwa) wakawatumikie vyema Wananchi kwani lengo
kubwa la Serikali ni kuona jamii inapata huduma bora ya Afya.
Dkt.
Semistatus Mashimba aliyazungumza hayo alipokuwa anafungua mafunzo ya
siku mbili ya Maafisa uandikishaji wa CHF wa vijiji vyote vya wilaya ya
Chemba kwa kushirikiana wadau wa mradi wa HPSS-Tuimarishe afya kuanzia
Tarehe 16 mpaka 17 Julai 2018 katika ukumbi wa Godown mjini Chemba.
“Nawaomba
muwe mabolozi wazuri kwa wilaya ya Chemba kwa kupunguza malalamiko na
kutoa elimu ya kutosha juu ya mabadiliko ya bei ya uandikishaji wa
kitambulisho cha bima ya Afya ya CHF Iliyoboreshwa kutoka tsh 13,000/=
kwenda tsh 30,000/=, na lengo kubwa la serikali ni kuwasaidia wananchi
hasa walio kwenye hali ya chini kupata huduma za afya katika vituo
mbalimbali vya afya vilivyoko nchini” aliongeza kwa kusema hivyo
Dkt.Semistatus Mashimba.
Naye
Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF Iliyoboreshwa) wilaya ya Chemba
Ndg. Haruna Haji amesema katika zoezi la uandikishaji Wilaya ya Chemba,
atahakikisha kwanza anatoa elimu ya kutosha kwa Maafisa Uandikishaji wa
Mfuko wa CHF katika kila kijiji ili kuondokana na vikwazo kwa wanachama
wa CHF na pia atahakikisha elimu hii muhimu ya bima ya afya inawafikia
wananchi wote wilayani hapo.
Ndg.Haji
amesema “katika uhifadhi wa nyaraka kuna utunzaji mkubwa na kuendelea
kuwahamasisha kukusanya fedha kamili kabla ya kutoa kitambulisho pia
tunaendelea kutoa elimu kwa wananchi maboresho yanayoendelea ya CHF
ikiwemo bei mpya ya kitambulisho cha CHF.
Vilevile
Afisa wa Mradi wa HPSS- Tuimarishe afya wilaya ya Chemba bi. Salome
Chilongani ametoa shukurani zake kwa mkuu wa wilaya pamoja mkurugenzi wa
halmashauri ya Chemba kwa kuonesha ushirikiano wao mkubwa kwenye
mafunzo hayo.
Bi.
Salome amesema “Kwanza nianze kwa kutoa pongezi na shukurani kwa
viongozi wetu wa wilaya ya Chemba, yaani mkuu wa wilaya pamoja na
mkurugenzi wa halmashauri, kwa kuonesha ushirikiano mkubwa sana kwenye
mafunzo haya, kwakweli wameshiriki kikamilifu sana na wameweza
kuwaelewesha Maafisa Uandikishaji hawa umuhimu wa elimu waliyoipata na
kutoa msisitizo kuilinda dhamana waliyoibeba.
Mimi kama mdau
nimefarijika kuona jinsi viongozi hawa walivyotupokea na kujali shughuli
zinazotekelezwa na mradi wa HPSS, nina matumaini mwaka mmoja baada ya
mafunzo haya tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa na tutakuwa na wanachama
wengi sana wa CHF katika wilaya yetu ya Chemba”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...