Mawaziri kutoka Wizara Tano zinazohusika na utekelezaji wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanzania, wamekutana na wataalam wa Tanzania walio katika Timu ya Kitaifa ya Majadiliano ya mradi ili kupata taarifa ya  utekelezaji wa mradi huo unaotarajiwa kukamilika mwaka 2020.
Kikao hicho  kilichoongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kimefanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dodoma ambapo Mawaziri waliohudhuria kikao hicho ni  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba,  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Dkt. Angeline Mabula,  Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira,  Antony Mavunde na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,  Dkt. Ashatu Kijaji.
Viongozi wengine  waliohudhuria ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua,  Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Usimamizi wa Bandari, Mhandisi Karim Mataka na  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo  ya Petroli Tanzania (TPDC),Mhandisi Kapuulya Musomba.
Pamoja na  kupata taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Bomba la Mafuta kutoka katika Timu hiyo ya Taifa ya Majadiliano (GNT), Mawaziri hao pamoja na wataalam mbalimbali walijadili changamoto  mbalimbali pamoja na utatuzi wake lengo likiwa ni kutekeleza mradi huo kwa ufanisi ndani ya muda uliopangwa.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ( wa Nne kulia), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (wa Tatu kushoto),  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Dkt. Angeline Mabula (wa Tatu kulia),  Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira,  Antony Mavunde (wa kwanza kulia) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,  Dkt. Ashatu Kijaji (wa Pili kulia) wakiwa katika kikao kilichokuwa kikijadili mradi wa Bomba la Mafuta jijini Dodoma.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ( katikati), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (kulia kwa Waziri wa Nishati),  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Dkt. Angeline Mabula (kushoto kwa Waziri wa Nishati),  Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira,  Antony Mavunde (haonekani pichani) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,  Dkt. Ashatu Kijaji (haonekani pichani) wakiwa katika kikao kilichokuwa kikijadili mradi wa Bomba la Mafuta jijini Dodoma. Wengine ni Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi mbalimbali za Serikali.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...