Na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Abdalla Hamisi Ullega amefanya ziara mkoani Kilimanjiro kwa kutembele jumla ya viwanda vya ngozi vitatu na wadau wengine wa sekta ya mifugo.

Katika ziara hiyo Mmiliki wa Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi cha Himo Tanners & Planters LTD Waiso amemweleza Naibu Waziri kuwa changamoto iliyopo kwa sasa katika kiwanda hicho ni pamoja na tozo nyingi zisizo na tija ambazo zinatozwa kuanzia Serikali ya kijiji mpaka Serikali Kuu. 

"Tozo zimekuwa nyingi mno katika Viwanda,ambapo inafikia wakati kiwanda kinashindwa kujiendesha kwa Ufanisi kwa sababu ya Muda na gharama za kufuatilia tozo hizo katika mamlaka husika,"amesema Waiso.

Aidha Waiso ametaja baadhi ya tozo hizo kuwa ni pamoja na Service Levy,Export Permit,Business Licence,Water use fee,Water right fee na Chemical Permit fee. 

Pia Ulega alipata fursa ya kutembele kituo cha Utafiti wa Mifugo, West Kilimanjaro (TALIRI), kiwanda cha kusindika ngozi cha Moshi Leather industries limited,Shamba la mifugo Kafoi,Watengenezaji wa chakula cha Mifugo, Marenga Millers Company LTD na kushuhudia uwekezaji mkubwa wa Shamba la Kuzalisha Kuku wazazi la The Irvines Group katika Halmashauri ya Siha.
Naibu waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega (wapili kulia) akiwa ameambatana na Mmiliki wa kiwanda cha ngozi Himo Tanners & Planters LTD , akipewa maelezo namna viatu vinavyotegenezwa kwa ngozi katika kiwanda hicho kilichopo mkoa wa Kilimanjaro.
Wanachi wa kijiji cha Lekirumuni wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifungo Mhe.Abdallah Ulega katika mkutano uliofanyika kata ya Ndinyika wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi Abdallah Ulega (kijani) akitembelea Shamba la mifugo la Serikali (NARCO)
Naibu waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa ameambatana na Mmiliki wa kiwanda cha ngozi  Himo Tanners & Planters LTD   akikagua ngozi kiwandani katika kiwanda hicho kilichopo mkoa wa Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na  wananchi katika mkutano uliofanyika cha kijiji cha Lekirumuni kata ya Ndinyika  wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...