Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Puma Energy Tanzania leo imekabidhi kwa Rais John Pombe Magufuli gawio la sh bilioni 9 kwa Rais John Pombe Magufuli ikiwa ni sehemu ya gawio la sh bilioni 18 kwa mwaka 2017 ambalo kampuni hiyo imetoa kwa wanahisa wake ambao ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Puma Investments Limited. 

Kampuni hiyo inamilikiwa kwa pamoja na serikali ya Jamhuri ya Muungano (Kupitia Msajili wa Hazina, Wizara ya Fedha) pamoja na Puma Investments Limited, kila moja ikiwa na umiliki wa hisa kwa asilimia 50 na hivyo kupitia gawio hilo kila mwanahisa amepata shilingi bilioni tisa (9).

Akizungumza,kwa niaba Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Limited Philippe Corsaletti, Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania Bw Lameck Hiliyai alisema kutokana na utendaji mzuri wa kampuni ya Puma Energy, gawio limekua kwa asilimia 100% ikilinganishwa na gawio la mwaka 2015 na kwa asilimia 29% ikilinganishwa na gawio na mwaka 2016.

Kwa mujibu wa Hiliyai, kufikia mwisho wa mwaka jana kampuni ilitengeneza faida kabla ya kodi ya jumla ya Shilingi 31 bilioni huku ikiwekeza takribani shilingi 9 bilioni kununua na kuendeleza miundombinu ikiwemo kununua vituo viwili vya mafuta kwenye jiji la Dodoma ikiwa ni juhudi za kuiunga serekali mkono katika kuhamia Dodoma.

“Ukuaji huu unaendana sambamba na mikakati ya kampuni ya kuhakiksha kampuni inaendelea kukua, kutengeneza faida, kukuza ajira nchini, kuchangia pato la taifa kupitia kodi, na kuendelea kuiunga serekali mkono katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo,’’ alisema.
 Rais John Pombe Magufuli  (katikati) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh bilioni tisa ikiwa ni sehemu ya gawio la sh bilioni 18 ambalo kampuni hiyo imetoa kwa wanahisa wake ambao ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  pamoja na Puma Investments Limited wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dr Phillip Mpango  (kushoto kwake), Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo Bw Prof Joseph Buchweshaija (kushoto) na Meneja Uendeshaji wa  Kampuni ya Puma Energy Tanzania Bw Lameck  Hiliyai (kulia)
 Meneja Uendeshaji wa  Kampuni ya Puma Energy Tanzania Bw Lameck  Hiliyai (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh bilioni tisa kwa Rais John Pombe Magufuli  (katikati) ikiwa ni sehemu ya gawio la sh bilioni 18 ambalo kampuni hiyo imetoa kwa wanahisa wake ambao ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  pamoja na Puma Investments Limited. Hafla hiyo fupi imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dr Phillip Mpango  (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo Bw Prof Joseph Buchweshaija.



 Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Puma Energy Tanzania Bw Prof Joseph Buchweshaija (kushoto) akipokea mkono wa pongezi kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Phillip Mpango wakati wa hafla ya makabidhiano hayo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...