Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Nyota wa Kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Arsenal ya Uingereza, Mesut Ozil  (pichani) ametangaza kustaafu kucheza timu ya taifa ya nchi hiyo kwa kile alichodai ni Ubaguzi na kutoheshimiwa na Shirikisho la Soka nchini humo (DFB).
Ozil na mwenzake anayekipiga na Manchester City, Ilkay Gundogan wote wana asili ya Uturuki na walionekana katika picha ya pamoja wakiwa na Rais wa hiyo, Recep Tayyip Erdogan. Picha hiyo imeleta mzozo kwa kuhusishwa na masuala ya Kisiasa. Hata hivyo, Ozil kupitia Ukurasa wake wa Twitter ametoa taarifa iliyokuwa ikikanusha shutuma hizo.
Katika taarifa hiyo, Ozil amevishutumu Vyombo vya Habari nchini Ujerumani haswa Magazeti kwa kuandika vibaya dhidi yake kuhusu picha ya pamoja na Rais Erdogan pamoja na kuwashutumu Wadhamini wa Shirikisho la Soka nchini humo. Moja ya sehemu ya taarifa hiyo Ozil ameelezea kuwa Mama yake amefundisha asisahau alipotoka, na kudai angewakosea heshima Waturuki endapo angekataa kupiga picha ya pamoja na Rais wao'.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa baadhi ya Magazeti nchini Ujerumani yamekuwa yakiandika kuhusu picha hiyo na Rais wa Uturuki na kuhusisha  na masuala yake (Erdogan) ya Kisiasa nchini humo.
Ozil katika miaka tisa akiwa na timu ya taifa ya Ujerumani amecheza michezo 92 katika kikosi cha timu ya taifa nakufunga mabao 23. Pia alikuwa moja wapo ya Wachezaji walioipeleka Ujerumani Kombe la Dunia 2014 pia kuivusha hadi Nusu Fainali ya Kombe la Ulaya 2012 na 2016, alikuwa na Kikosi hicho kwenye Michuano ya Kombe la Dunia 2010 na 2018.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...