SHULE ya Sekondari St. Anne Marie Academy imefanikiwa kuwa ya kwanza kitaifa kwenye somo la uhasibu katika matokeo ya kidato cha sita.


Pia shule hiyo imefanikiwa kushika nafasi ya pili kitaifa kwenye masomo ya biashara katika matokeo yaliyotangazwa mwishoni mwa wiki Zanzibar na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA).



 Akizungumza na Michuzi Blog, Mkuu wa shule hiyo, Gladius Ndyretabura amesema wanafunzi wake wote 100 waliofanya mtihani huo wamefanikiwa kupata sifa za kujiunga na Vyuo vikuu mbalimbai nchini na nje ya nchi.



 Amesema shule yake imefanikiwa kutoa wamnafunzi 54 kwa daraja la kwanza na la pili.Pia imetoa wanafunzi 45 wa daraja la tatu na kwamba hakuna hata mwanafunzi mmoja aliyepata daraja la mwisho yaani 0.



 Amesema hiyo si mara yake ya kwanza kwa shule yake kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa kwani hivi karibuni Mkoa wa Dar es Salaam uliipatia Ngao Maalum shule hiyo kama sehemu ya kutambua mchango wake katika kuinua elimu hapa nchini na kuwa miongoni mwa shule zinazofanya vizuri kitaaluma.



 Amesema shule yake ilipewa ngao inayoonyesha kuwa ni miongoni mwa shule zilizofanya vizuri zaidi kwenye matokeo ya darasa la saba Best Performing Primary School in Tanzania.



 Ameongeza shule yake pia ilifanikiwa kuingia 10 bora kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka jana na kwamba nia yake ni kuwa namba moja kitaifa kwenye matokeo yanayokuja.



Amesema kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka jana walifanikiwa kuwa wa kwanza katika Wilaya ya Ubungo, wamekuwa wa pili Mkoa wa Dar es Salaam na walikuwa wanane kitaifa sasa.


"Hii haitufanyi tubweteke tutapambana kupata nafasi za juu zaidi,"amesema.
Mkuu wa shule ya Sekondari St Anne Marie Academy ya Mbezi kwa Msuguri Dar es Salaam,  Gladius Ndyetabura akiwasomea matokeo ya kidato cha sita wanafunzi wa shule hiyo ambapo shule hiyo imefanikiwa kuongoza kitaifa kwenye somo la uhasibu na kuwa ya pili kitaifa kwenye masomo ya biashara.
 Mkuu wa shule ya Sekondari St Anne Marie Academy ya Mbezi kwa Msuguri jijini Dar es Salaam, Gladius Ndyetabura akifurahia matokeo ya kidato cha sita na wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kutangazwa ambapo shule hiyo imeongoza kitaifa kwenye somo la uhasibu na somo la biashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...