Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana
na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amempa mwezi mmoja mkandarasi anayejenga kwa kiwango cha lami barabara yenye urefu wa kilometa mbili inayo unganisha Daraja la Nyerere na barabara ya Kibada -Feri iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, kukamilisha kazi hiyo hadi tarehe 31 Agosti mwaka huu ili kurahisisha mawasilino kwa wananchi wanao tumia daraja hilo.

Waziri Mhagama ameyasema hayo hapo jana tarehe 19 Julai 2018, alipotembelea katika daraja la Nyerere ili kukagua ujenzi wa barabara hiyo na uendeshaji wa shughuli katika daraja la Nyerere ambapo amesema serikali kutokamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo kunasababisha kero kwa wananchi wanaovuka kwa miguu na wanaovuka kwa kutumia vyombo vya usafiri kushindwa kupita kwa urahisi, hali inayochangia kupungua kwa mapato yanayokusanywa darajani hapo.(PAUSE-INSERT)

Kwa upande wao Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio na Mkandarasi wa barabara hiyo, Mhandisi Jamal Mruma wote kwa pamoja wamemuhakikishia Waziri Mhagama kutekeleza maagizo hayo kwa wakati ili kuondoa usumbufu uliopo kwa sasa katika daraja na kuweza kuongeza makusanyo ya mapatokatika daraja hilo.

Mbali na gaizo hilo la kukamilishwa kwa barabara , pia
Waziri Mhagama amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF kuhakikisha unawekwa mfumo bora wa utambuzi wa vyombo vya usafiri vinavyovuka darajani hapo ili kujua gharama halisi ya tozo ya vyombo vinavyovuka na kuepuka upotevu wa mapato kutokana na kutokuwa 
na mfumo wenye kutambua tozo halisi kwa vyombo hivyo.

Daraja la kigamboni tangu lianze kufanya kazi mwezi Mei mwaka 2016
hadi mwezi Juni 2018, mpaka sasa limeingiza mapato ya takiribani shilingili bilioni 17.1 mapato hayo yanayotokana na tozo kwa vyombo vya usafiri vinavyopita katika daraja hilo.

Imetolewa na Afisa Uhusiano wa Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF
Angella Msangi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...