Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia  Profesa Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa kukabidhi magari 47 kwa ajili ya wathibiti wa  ubora wa  Shule  wa Kanda na Wilaya na magari  mawili  kwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) katika hafla iliyofanyika hapa Mjini Dodoma.
 Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia  Profesa Joyce Ndalichakoakikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa magari hayo kwawathibiti  wa ubora wa  Shule  wa Kanda na Wilaya na magari  mawili  kwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) katika hafla iliyofanyika hapa Mjini Dodoma.
 Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia  Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika gari mara baada ya kuzindua
Sehemu ya magari ya wathibiti wa  ubora wa  Shule  wa Kanda na Wilaya na magari  mawili  kwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia  Profesa Joyce Ndalichako amekabidhi magari kwa ajili ya kuimarisha Uthibiti wa ubora elimu.
Jumla ya magari hayo ni 47, ambapo  magari 45 ni kwa ajili ya wathibiti ubora wa  Shule  wa Kanda na Wilaya na magari  mawili  kwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).
Akizungumza wakati wa kukabidhi magari hayo mjini Dodoma Profesa Ndalichako amesema  wathibiti ubora  wa shule kutumia  magari hayo   kwa malengo yaliyokusudiwa na hatua kali zitachukuliwa kwa wale watakaotumia magari hayo kinyume na malengo yaliyokusudiwa.
Amesema kwa mujibu wa Dira yetu ya Maendeleo, Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano na Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 Tanzania inalenga kujenga uchumi wa Viwanda ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Profesa Ndalichako amesema kufikia malengo ya uchumi wa kati  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ndiyo yenye dhamana ya kusimamia utoaji elimu, ujuzi, maarifa na stadi zitakazowawezesha vijana wetu kutoa mchango unaotakiwa katika ujenzi wa uchumi wetu.
Aidha Wizara itasimamia vyema elimu na mafunzo yatolewayo ili kuhakikisha yanakuwa bora na yanatoa mchango wenye tija katika ujenzi wa uchumi wetu.  
“Ninathubutu kusema kuwa Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inasimamia kwa dhati kabisa jukumu hili la utoaji wa elimu bora kwa kununuaa pikipiki 2,894 ambazo zimesambazwa kwenye Halmashauri 156 katika mikoa 25 kwa ajili ya kusaidia  Waratibu Elimu Kata katika kutekeleza majukumu yao ili kuhakikisha kuwa elimu bora inatolewa shuleni katika maeneo yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...