Na Ramadhani Ali, Maelezo Zanzibar
Mamlaka ya Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) imejidhatiti kuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingizwa nchini zinawafikia wananchi zikiwa salama kwa matumizi kwa lengo la kulinda afya zao.

Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Usalama wa chakula wa ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar alieleza hayo katika jaa la Kibele wakati wa kazi ya kuangamiza tani 95 za bidhaa za mchele, sembe na Unga wa ngano pamoja na tani moja ya dawa za binadamu.

Alisema bidhaa za chakula zilizoangamizwa za mfanyabiashara Mohamed Mattar ziliharibika baada ya kuhifadhiwa kwa muda mrefu katika maghala yasiyorasmi na yaliyokosa sifa za kutumika kwa kazi hiyo.

Dkt. Khamis alieleza kuwa kutokana na maghala hayo kukosa viwango vinavyokubalika na kutosajiliwa na ZFDA, mfanyabiashara Mattar alikuwa  akiweka bidhaa zake kwa siri wakati wa usiku.

Akitaja viwango vya bidhaa zilizoangamizwa, Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti na uhifadhi wa chakula wa ZFDA alisema mchele ulikua tani 52, unga wa ngano tani 37 na sembe ilikuwa tani sita.
  Fundi wa mageti akikata geti la Ghala lililokua likihifadhiwa bidhaa za Mchele, Unga wa ngano na sembe uliomaliza muda na haufai kwa matimizi ya binadamu katika mtaa wa Migombani Mjini Zanzibar.
 Sshemu ya bidhaa ya Mchele na Unga wa Ngano na Sembe zikiteremshwa katika magari kwa ajili ya Kuangamizwa katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Unguja.
 Dawa za binadamu za aina mbali mbali za kuondosha maumivu na Virutubisho zilizo angamizwa katika  Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
 Gari la Kijiko likiangamiza Dawa za kuondosha maumivu na Virutubisho zilizoangamizwa katika  Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkurungezi Idara ya Udhibiti na Usalama wa Vyakula wa ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar akizungamza na Waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuangamizaji Bidhaa zisizofa kwa Matumizi ya Binadamu lililofanyika katika  Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Picha na Abdalla Omar Maelezo  -  Zanzibar.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...