Jamii imetakiwa kufahamu kuwa Kamati za Mazingira katika ngazi zote zipo kwa mujibu wa Sheria, Sheria ya Mazingira kifungu Na. 38 (1-2) na Kamati hizo zina wajibu wa kusimamia mazingira kikamilifu yanayohusu maeneo yao.

Akizungumza na Watendaji wa Mkoa wa Tabora katika hafla ya kuzindua Kamati ya Usimamizi wa mazingira Mkoani hapo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameahidi kujenga uwezo kwa watendaji hao kwa kuwapatia mafunzo.

Aidha, Waziri Makamba amesisitiza unaziswaji kwa Kamati za Mazingira katika ngazi za vitongoji, vijiji na kata nchi nzima na kuahidi kutuma wataalamu kutoa mafunzo kwa kamati hizo ili ziweze kujua majumu yao ipasavyo na kusema kuwa shughuli za hifadhi za mazingira hazitafanikiwa kama Kamati za mazingira hazitatimiza majukumu yake katika ngazi hizo.

Waziri Makamba amesema kuwa dunia tunayoishi sasa tumeiazima kwa kizazi kinachokuja hivyo hatuna budi kuitunza. “Ukiazima kitu kwa mtu yeyote huna budi kukitunza na kukulinda ila kukirudisha kwa mwenyewe kikiwa katika hali nzuri.” Makamba alibainisha.

Katika wakati mwingine Waziri Makamba ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Tabora kuteua ama kuajiri Maafisa wa mazingira wa kutosha ili kusimamia kikamilifu uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira, pamoja na kuandaa mpango tekelezi wa mazingira katika ngazi ya Mkoa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na mamia ya wakazi wa Mkoa wa Tabora (hawapo pichani) waliojitokeza katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kumsikiliza. Waziri Makamba amezindua Kamati ya Mazingira na kuwataka wananchi hao kuwa mstari wa mbele kusimamia masuala ya mazingira katika maeneo yao
Wakazi wa Kijiji cha Igambilo Kata ya Misha Mkoani Tabora waishio pembezoni mwa Bwala la Igombe wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (hayupo pichani) mara baada ya kutembelea Kijiji chao na kuzungumza nao umuhimu wa kuendelea kutunza Bwawa la Igombe. Waziri Makamba ameahidi kutoa mifuko 100 ya Saruji kuchangia ujenzi wa Zahanani Kijijii hapo.
Bwala la Igombe ambalo ni chanzo kikubwa cha maji kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora, shughuli zisizoendelelevu za kibinadamu zinapelekea kupungua kwa kina cha bwana hilo kila siku. Waziri mwenye dhamana ya Mazingira Mhe. January Makamba ametembelea eneo hilo na kuagiza wananchi wanaozuia maji kwa kutumia mabanio kuondolewa mara moja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...