MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo amewaonya walanguzi wa korosho kutoka kwa wakulima wilayani humo kuacha tabia hiyo mara moja kabla hawajakumbana na mkono wa sheria.

Badala ametaka ufuatwe utaratibu ambao umewekwa wilayani humo wa korosho hiyo kukusanywa kwenye maghala na kuuzwa kwa utaratibu uliopagwa ili mkulima aweze kunufaika na kilimo chake.

Hayo yalisemwa wakati akizungumza na mtandao huu ambapo pia aliwahimiza wananchi wilayani humo kujikita kwenye kilimo cha zao la korosho ili kunufaika nacho kutokana na uwepo wa soko la uhakika.Alisema ili kuhakikisha wanafanikisha kwenye jitihada hizo tayari wamegawa miche ya mikorosho bure 62050 ambako wananchi wamehamasika kupitia hekta 152.

Alisema pia kupitia amcos zao zamani zilikuwa zimelala lakini hivi sasa zimefufuka kutokana na kuwepo uhamasishwaji huo ambao umewawezesha kutambua umuhimu wa kilimo hicho .“Ndugu zangu wananchi limeni korosho kwani ni moja kati ya zao linalopewa kipambele na serikali ya awamu ya tano na tayari soko lake ni la uhakika hivyo walitilie mkazo kwa lengo la kunufaikanalo”Alisema DC Muheza.

Aidha alisema wilaya hiyo tayari dawa zipo kwa ajili ya wakulima hivyo watumie dawa zilizosambazwa ili kuwawezesha kulima kilimo chenye tija na cha kisasa ambacho kitawainua kimaisha.Hata hivyo aliwataka maafisa ugani watoke ofisini waende kwa wakulima kuhamasisha wananchi kutumia  dawa hizo kadiri ya vipimo vinavyohitaji ili waweze kulima kilimo chenye tija na manufaa kwao ili kuwaezesha wakulima kunufaika.

“Huko kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara kumekuwa na ulanguzi kwenye manunuzi ya korosho hizo lakini kwetu hilo halipo ila nitoe wito kwa wale ambao wanafikiria kufanya biashara hivyo kinyume na utaratibu wao kama viongozi,serikali hawatakuwa tayari yoyote ambaye atataka kununua korosho kwa wakulima kwa bei za ulanguzi hivyo tutahakikisha anachukuliwa hatua “Alisema DC Muheza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...