Na Shani Amanzi,Chemba

MKUU wa Wilaya ya Chemba Saimon Odunga amewataka wananchi wa kitongoji cha Lalalami katika Kijiji cha Itolwa waache mara moja mgogoro wa kung’ang’ania kuwa wapo eneo la Wilaya ya Kiteto.

Badala yake amewataka wajue kabisa bado wapo wilayani Chemba kwani Serikali inafata ramani ambayo inatambulika.

Odunga amesema wanatambua kabisa kitongoji cha Lalalami kipo mpakani kati ya Wilaya ya Chemba na wilaya ya Kiteto ambapo mgogoro ulianza kuanzia mwaka 2012 na mwaka 2016 kupitia Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia vifungu vyake vya sheria ya ardhi waliamua Kitongoji cha Lalalami kuwa wilayani Chemba."Lakini bado wananchi wakakataa maamuzi hayo na ukweli ndiyo huo. Leo hii ni mara ya tatu mwaka 2018 Serikali imeamua kukaa chini na wananchi tena kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Magesa ,Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Chemba na Kiteto .

"Wataalam wa Halmashauri za Wilaya zote na kufanya maamuzi ya pamoja ya kuzuia kabisa mgogoro huo wa mara kwa mara wa wananchi kukataa kuwa eneo la Serikali ya Wilaya ya Chemba na atayekwenda kinyume hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa sababu serikali haiwezi kupoteza muda na fedha kusuluhisha mgogoro ambao ukweli unajulikana,” amesisitiza Odunga.

Aidha Odunga amesema “tunajua sababu kubwa ni shughuli za kiuchumi ambapo jamii iliopo inafanya shughuli za ufugaji na mnataka kujumuika na jamii yenzenu ya Kiteto ya Ufugaji lakini wilaya ya Chemba wengi wao ni wakulima." Lakini mkumbuke jamii zote hizi mbili za wakulima na wafugaji zipo wilayani Chemba na huwa wanafata kanuni na taratibu za ufugaji na kilimo ili kuzuia migogoro ya ardhi,wakulima na wafugaji ambapo ni janga la nchi nzima,"amesema.

Odunga alifanya ziara ya siku moja kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Magesa ambayo ilikuwa Agosti 21 mwaka huu ambapo walikuwa wanasuluhisha mgogoro kati ya wilaya na wilaya kati ya Chemba na Kiteto.
MKUU wa Wilaya ya Chemba Saimon Odunga akizungumza na Wanachi wa kitongoji cha Lalalami katika Kijiji cha Itolwa,kuhusua kuacha mara moja mgogoro wa kung’ang’ania kuwa wapo eneo la Wilaya ya Kiteto,na badala yake amewataka wajue kabisa bado wapo wilayani Chemba kwani Serikali inafata ramani ambayo inatambulika.Katika mkutano huo DC wa Chemba aliambatana na DC wa Kiteto pamoja na maofisa mbalimbali wa wakiwemo wa Ulinzi na usalama,kuhakikisha mgogoro huo unatatuliwa.



Baadhi ya wananchi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa kitongoji cha Lalalami katika Kijiji cha Itolw,wilayani Chemba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...