Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Naibu Waziri na Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Jimbo la Abdallah Ulega amefunga mafunzo ya siku mbili ya ufugaji wa kuku kwa Baraza la  wakina mama wa Jimbo la Mkuranga Mkoa wa Pwani.

Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na kampuni ya AMK Gliters inayojihusisha na ufugaji wa kuku yalianza jana yakihudhuriwa na jumla ya wakina mama 326 kutoka kata mbalimbali za Mkuranga.Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Ulega amesema kuwa anatarajia kuona wakina mama wa jimbo la Mkuranga wanafuga kuku kwa ajili ya maendeleo pamoja na kukuza kipato chao.

Ulega amesema kuwa, elimu waliyoipata ya ufugaji wa kuku wa kibiashara utawasaidia wananchi hao kujiendeleza zaidi kiuchumi na kuwapa hamasa kuwa majukwaa kama haya yana faida kubwa kwa maendeleo ya Mkuranga.

Amesema, mafunzo ya ujasiriamali  kama haya yanawezekana ila changamoto kubwa imekuwa ni kufika kwa wakina mama hao kutokana na umbali wanapokaa ila amewaomba wasikate tamaa na kumtaka Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Jimbo la Mkuranga Mariam Ulega  kutoa taarifa ili wadau mbalimbali wawezw kujitokeza kuwawezesha pindi zinapojitokeza.

Hata hivyo Ulega, amemtaka Mwenyekiti Wa Baraza kuhakikisha vikundi vilivyojiandikisha tayari kuwa na akaunti za benki ili kuwe na nidhamu ya fedha hususani  usimamizi mzuri.Ameongezea kuwa, tayari ameshapata cherehani 50 na majora kwa ajili ya kuwapatia wakina mama na kila kata watapata cherehani 2 ikiwa ni njia nyingine ya kujiinua kiuchumi.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, (Mb) wa Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wajasiria mali katika kongamano la uwezeshaji kiuchumi lililo fanyika mkoni Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akisalimiana na Meneja wa CRDB Bank Tawi la Mbagala, Midlaster Nsanzugwanko.
Sehemu ya wajasiliamali mara wakiendelea na kongamano lililo fanyika mkoa wa Pwani.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...