Na Catherine Francis –Mahakama Kuu Arusha

Jaji Mfawidhi mpya wa Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha, Mhe. Mosses Mzuna amekabidhiwa rasmi Kanda hiyo ya Mahakama na aliyekuwa Kaimu Jaji Mfawidhi, Mhe Jaji Sekela Moshi.

Makabidhiano hayo yamefanyika mapema Agosti 16 katika kikao cha utambulisho wa wahe.Majaji wapya pamoja na Jaji Mfawidhi ambayo pia yalihudhuriwa na baadhi ya Watumishi wa Mahakama.

Katika kikao hicho Mhe Jaji Moshi aliwasisitiza watumishi wa Mahakama Arusha kuendeleza ushirikiano, uwajibikaji na kufanya kazi kwa malengo kwani hiyo ndiyo sababu inayoifanya Arusha kuwa kanda ya mfano kwa mafanikio.Jaji Sekele aliendelea kuwahimiza watumishi waache kufanya kazi kwa mazoea bali wajitume kwa bidii ili kuweza kuondoa kabisa mlundikano wa kesi Mahakamani.

Kwa upande wake, Mhe Jaji Mzuna alimshukuru Mhe Jaji Moshi kwa mapokezi mazuri aliyoyaandaa yeye pamoja na viongozi wake, pia aliwaomba watumishi ushirikiano ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kila siku.Kwa kusisitiza hilo alinukuu usemi wa mwandishi John C Maxwell usemao “VALUE TEAM LEADERSHIP ABOVE INDIVIDUAL LEADERSHIP” akiwa na maana ya kuwa uongozi mzuri ni ule wa ushirikiano na siyo wa mtu binafsi.
Aliyesimama ni Jaji Mfawidhi Mhe Jaji Mzuna akiwa anazungumza na watumishi
Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha, Mhe Jaji Mosses Mzuna (katikati), kushoto ni aliyekuwa Kaimu Jaji Mfawidhi Mhe Jaji Sekela Moshi na Mhe. Jaji Thadeo Mwenempazi walipokuwa wakizungumza na Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Arusha (hawapo pichani).
Mhe Jaji Thadeo Mwenempazi akizungumza jambo na Watumishi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...