Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas E Mwangela akikagua ujenzi wa daraja la Kikamba linalounganisha kata ya Kapalala na Gua Wilayani Songwe, katika ziara yake ya siku mbili wilayani humo aliyoianza leo. Daraja hilo limeanza kujengwa Oktoba 20, 2017 na linatarajiwa kukamilika Septemba, 2018 likiwa limegharimu shilingi bilioni 1.4.
Ujenzi wa daraja la Kikamba linalounganisha kata ya Kapalala na Gua Wilayani Songwe ukiendelea, Daraja hilo limeanza kujengwa 20 Oktoba, 2017 na linatarajiwa kukamilika Septemba, 2018 likiwa limegharimu shilingi bilioni 1.4.

Na Grace Gwamagobe, Songwe

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas E Mwangela amekataa ombi la Mkandarasi kutoka kampuni ya Mats Engineering Ltd Paulo Philipo Paulo la kuongezewa kipindi cha miezi miwili ili aweze kukamilisha ujezi wa Daraja la Kikamba Wilayani Songwe.

Brigedia Jenerali Mwangela amekataa ombi hilo leo alipokagua ujenzi wa daraja la Kikamba linalounganisha kata za Kapalala na Gua wilayani Songwe kwakuwa sababu alizotoa mkandarasi huyo hazijitosheleji.

Amesema daraja hilo lazima likamilike kwa muda uliopangwa ambao ni Septemba, 2018 huku mkandarasi huyo akitoa sababu kuwa atachelewa kukamilisha ujenzi huo kutokana na mvua nyingi zilizonyesha na mwamba mgumu uliopo eneo la ujenzi.

“Mkandarasi ahakikishe anafanya kazi mchana na usiku ili akamilishe ndani ya muda wa mkataba, vifaa vya kumuwezesha kufanya hivyo anavyo na ombi la kuongezewa muda wa ujenzi mimi siafikiani nalo”, amesema Brigedia Jenerali Mwangela.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samuel Jeremia amesema yeye na viongozi wengine wataendelea kusimamia miradi ya maendeleo na katika ujenzi wa daraja hilo watahakikisha wanamsimamia mkandarasi huyo ili amalize ndani ya muda uliopangwa.

Daraja la Kikamba linaolunganisha kata za Kapalala na Gua limeanza kujengwa mwezi Oktoba 2017 na linatarajiwa kukamilia Septemba 2018 likiwa limegharimu shilingi bilioni 1.4.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...