Brigadia Jenerali Mary Hiki akizungumza na wanamichezo kutoka (Tanzania hawapo pichani) washiriki wa Tamasha la Kwanza la Michezo la Afrika Mashariki linaloendelea jijini Bujumbura, Burundi. Brigadia Generali Hiki ambaye anahudumu katika Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi alizungumza na wanamichezo hao kwaniaba Kaimu ya Balozi. Tamasha hili linalofanyika kwa mara ya kwanza nchi Burundi limetokana na maagizo ya Mkutano wa 35 wa Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki.

Tamasha hili lenye kauli mbiu "kujenga Jumuiya ya Afrika Mashariki na amani kupitia michezo" linafanyika kuanzia terehe 16 hadi 30 Agosti, 2018. Washiriki zaidi 1000 kutoka nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki watashiriki kwenye michezo mbalimbali ya tamasha hili.

Tanzania imewakilishwa na jumla ya wanamichezo 58 ambao watashiriki katika michezo ya mpira wa pete, mpira wa miguu, riadha na karatee.

Tamasha hili limefunguliwa tarehe 16 Agosti 2018 na Mhe. Dkt. Joseph Butore Makamu wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Burundi, katika viwanja vya Sekondari vya SOS jijini Burundi na kuhudhuriwa na viongozi na watendaji waserikali kutoka nchi wanachama. 
Meza kuu ni Mhe. Dkt. Joseph Butore Makamu wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Burundi (wa pili kulia) Bw.Liberatus Mfumukeko (wapili kushoto) Katibu Mkuu Seretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ali Kirunda Kivenjija Naibu wa Pili wa Waziri Mkuu na Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki kutoka Uganda (wa kwanza kulia) na Mhe. Jacques Enyenimigabo Waziri wa Vijana na Michezo wa Burundi (wa kwanza kushoto) wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa wa Burundi ukipigwa kwenye hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Kwanza la Michezo la Afrika Mashariki.
Sehemu ya watendaji na viongozi wa Serikali wa nchi Wanachama wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa wa Burundi ukipigwa kwenye ufunguzi wa Tamasha la Michezo.
Wanamichezo kutoka Tanzania wakipita kwa furaha mbele ya jukwaa kuu kwenye hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Kwanza la Michezo la Afrika Mashariki.
Moja ya mchezo wa ufunguzi wa tamasha ukiwa unaneendelea jijini Bujumbura, Burundi.
Hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Kwanza Michezo la Afrika Mashariki ikiwa inaendelea.
Bw. Liberatus Mfumukeko Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki akihutubia kwenye hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Kwanza la Michezo la Afrika Mashariki linaloendelea jijini Bujumbura, Burundi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...