Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa tatu kushoto), waliokaa msitari wa mbele, akifuatilia mada iliyowasilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bi. Agnes Sitta Kijo (hayupo pichani).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bi. Agnes Sitta Kijo (wa kwanza kushoto), waliosimama, akiwasilisha mada inayohusu vigezo vya uanzishaji viwanda vya dawa nchini Tanzania kwa wadau wa kongamano la biashara la kimataifa, linalofanyikia Beijing Kempinski Hotel, Lufthansa Centre, Beijing – China.
Na Gaudensia Simwanza
– Dar es Salaam
TFDA
inaendelea na uhamasishaji wa wadau wa ndani na nje ya nchi katika kuanzisha
viwanda vya dawa nchini Tanzania. Hivi sasa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bi.
Agnes Sitta Kijo yupo nchini China kwa ajili ya kuhamasisha wadau mbalimbali wa
kimataifa kuja kufanya uwekezaji huo katika nchi yetu.
Katika
mada yake aliyoiwasilisha katika kongamano la kimataifa la wadau wa dawa
linalofanyikia katika Beijing Kempinski
Hotel, Lufthansa Centre, Beijing – China, aliwafafanulia wadau hao kuhusu
vigezo vya kisheria vinavyotakiwa na
kuwahakikishia wadau hao kwamba TFDA imeweka mazingira mazuri ya
uwekezaji wa tasnia ya dawa na kwamba mwekezaji yeyote atakayekidhi vigezo
hatakwamishwa bali atapewa ushirikiano kwa kuwa Tanzania ina dhamira ya dhati
katika uanzishaji wa viwanda hususan vya dawa.
Matarajio
ya TFDA kwa mikakati ya aina hii, ni kushuhudia uanzishwaji wa viwanda vya
bidhaa zinazodhibitiwa na taasisi hii kwa nia ya kutosheleza mahitaji ya soko
la ndani na nje ya nchi, kulinda afya ya jamii na kukuza uchumi wa nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...