Na Salum Vuai, ZANZIBAR 

JUKUMU la mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika mataifa ya nje, ni kuwaunganisha wananchi na sio kuwa karibu na serikali na viongozi pekee.

Kauli hiyo imetolewa na Balozi mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Dk. Ahmad Hamood Al Habsy, alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu wanaosomea diplomasia na uhusiano wa kimataifa walipomtembelea ofisini kwake Migombani mjini Unguja.

Balozi huyo alieleza kuwa, kwa kutambua hilo, amefungua milango ya ofisi yake kutoa fursa kwa wananchi mbalimbali wa Zanzibar pamoja na viongozi, kwenda kujifunza masuala muhimu kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya kihistoria kati ya nchi yao na Oman.

Alisema, baadhi ya watu wanadhani kwamba kufanya kazi katika ofisi za kibalozi kuna mipaka inayowatenganisha mabalozi na wananchi wa kawaida, jambo alilosema sio sahihi.

Dk. Al Habsy alisema licha ya mabalozi kuwajibika kiserikali katika mataifa wanayopelekwa kufanya kazi, pia wanapaswa kuwa karibu na wananchi wa nchi za nje wanazokuweko, wakitambua kuwa nayo ni sehemu ya majukumu yao. 
BALOZI Mdogo wa Oman anayefanya kazi zake Zanzibar Dk. Ahmad Hamood Al Habsy (Kulia), akizungumza na wanafunzi wanaosomea fani ya Diplomasia na Mahusiano ya Kimataifa, wakati walipofanya ziara kwenye ofisi za ubalozi huo zilizopo Migombani mjini Zanzibar.
DK. Ahmed Hamood Al Habsy, Balozi Mdogo wa Oman visiwani Zanzigar (Kulia) na Mhadhiri wa somo la Diplomasia na Mahusiano ya Kimataifa katika Chuo Kikuu Zanzibar kilichoko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja, Mohammed Yussuf.
WANAFUNZI, wahadhiri na baadhi ya maofisa wa Ubalozi Mdogo wa Oman mjini Zanzibar, wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mdogo Dk. Ahmad Hamood Al Habsy nje ya jengo la ubalozi huo Migombani, Zanzibar baada ya ziara ya wanafunzi hao iliyolenga kubadilishana mawazo na kujifunza shughuli za Kidiplomasia na Mahusiano ya Kimataifa. (PICHA ZOTE NA HAROUB HUSSEIN). 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...