Mtoto wa Kike mwenye umiri wa miaka  13, (Jina limehifadhiwa) ameunguzwa baada ya kumwagiwa mafuta ya taa na  kisha kuwashwa na kiberiti na mama yake mzazi.

Binti huyo amelazwa katika hosptali ya St, Joseph Mbweni katika wodi ya watoto akiwa hawezi hata kutoa maelezo  vizuri.

Akizungumza jinsi mtoto huyo alivyofikishwa hospitalini hapo, Dkt,  Valentino Francis Bangi amesema, mtoto alifikishwa hospitalini hapo alfajiri ya Agosti 31 kuamkia Septemba Mosi mwaka huu akiwa katika hali mbaya, alikuwa ameunguzwa na moto sehemu ya mbele ya  kifua na usoni.

Dkt, Bangi amesema, mtoto huyo alipofikishwa hospitalini hapo alikuwa hawezi kupumua wala kuongea, lakini walimpatia huduma ya kumuweka katika hali nzuri na kuanza kurudi katika hali ya ubinadamu .

Dkt. Bangi amesema moja ya huduma waliyoifanya ni kumuoongezea maji pamoja na kumpatia huduma nyingine ya kumfanya apumue.
‘kwa sasa hali ya mgonjwa, anaendelea vizuri tofauti na alivyokuwa kwa sababu alikuwa hawezi hata kuongea, lakini sasa hivi anazungumza ambapo amelazwa wodi ya watoto hospitalini hapa.


Kwa upande wake, Ofisa Ustawi wa Jamii, wa Hospitali hiyo,  Angela Isingo ambaye anashughulikia masuala ya watoto, amesema tukio hilo linasikitisha , kwani wamemuhoji  binti huyo amesema aliyemfanyia kitendo hicho ni mama yake mzazi.

Isingo amesema mtoto huyo ameeleza chanzo cha tukio hilo kwamba, “binti alirudi usiku kutoka shule, mama yake akamuuliza kibubu cha pesa kiko wapi?, kwa sababu ndani kulikuwa na vibubu viwili havionekani kwa hiyo akaenda moja kwa moja kwa huyo mtoto na kumuuliza, anasema mtoto alimjibu kuwa hafahamu kibubu kilipo, mama yake akaendelea kumuhoji tena kuwa akitafute hadi akipate, akasema akazunguka akapata kibubu kimoja, na pale  ndani haishi peke yake ana baba yake na  ndugu zake wawili na dada yake mkubwa mmoja.

Akasema licha ya kumjibu mama yake kuwa hafahamu kibubu hicho kilipo, mama yake akaendelea kumuhoji kuwa, lazima aseme kibubu kilipokwenda ndiyo mama yake akachukua mafuta ya taa akamwagia na  kisha  akachukua kiberiti kumuwasha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...