Na Mwandishi wetu
MRADI mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania umezinduliwa jana.
Akizindua mradi huo ofisi za Taasisi ya tafiti za kiuchumi na kijamii –ESRF, Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba alisema mradi huo unakuja wakati muhimu ambapo taifa linajikita katika kuelekea uchumi wa kati unaotegemea kilimo.
“Sekta ya kilimo imeendelea kuwa ni Sekta muhimu katika maendeleo ya uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla hususan katika wakati huu Tanzania inapojizatiti kuelekea uchumi wa viwanda,” alisema Waziri Tizeba huku akisema kwamba sekta ya Kilimo iimekuwa ikiendelea kukua kwa kuchangia asilimia 30 ya fedha za kigeni na kuchangia malighafi za viwanda kwa asilimia 65.
Mradi huo umezinduliwa takaribani miezi mitatu baada ya wizara kuzindua rasmi Program ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo awamu ya pili (ASDP II), yenye lengo la kuleta mageuzi ya Sekta ya kilimo (kilimo, mifugo na uvuvi) ili kuongeza uzalishaji na tija na kufanya kilimo kiwe cha kibiashara zaidi na kuongeza pato la wakulima wadogo.
Pamoja na kufanya uzinduzi huo aliipongeza ESRF na timu nzima ya mradi wa GCRF-AFRICAP kwa kuchangia maendeleo ya sekta ya kilimo kupitia tafiti na kujenga uwezo kwa lengo la kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabia nchi kwa makundi ya jamii yaliyokua kwenye hatari zaidi.
Alisema Wizara yake itaendelea kukuza na kulinda maendeleo ya sekta ya kilimo yaliyo endelevu, kwa kuongeza uzalishaji, kuboresha mifumo ya kilimo inayokwenda sambamba na mabadiliko ya tabia nchi.
“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inazingatia tatizo la mabadiliko ya tabia ya nchi kwa umakini mkubwa sana, na Tanzania ni miongoni mwa nchi chache Barani Afrika ambazo zimefanikiwa kuendeleza Mpango Mkakati wa Kupambana na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi, ili kwenda sambamba na dira ya maendeleo ya taifa 2025.” Alisema Dk. Tizeba.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Dk.
Charles Tizeba (hayupo pichani) na washiriki wakati wa hafla ya uzinduzi
wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za
kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar
es Salaam.
Mgeni
rasmi Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba akitoa hotuba kabla ya
kuzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za
kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar
es Salaam.
Mgeni
rasmi Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba (katikati) akizundua rasmi
mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko
ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na
mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano
wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam
huku Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii
(ESRF), Dk. Tausi Kida (wa pili kushoto), Msimamizi wa mradi wa AFRICAP
kwa Tanzania na Mkuu wa Idara ya Ushauri Elekezi –ESRF, Bi. Vivian Kazi
(kushoto), Mwakilishi wa, FANRPAN – AFRICAP anayeshughulikia sera
(kikanda), Bi. Sithembile Ndema Mwamakamba (wa pili kulia) pamoja na Dr.
Susanna Sally (kulia) kutoka Chuo Kikuu cha Leeds nchini Uingereza
wakishuhudia tukio hilo.
Dr.
Susanna Sally kutoka Chuo Kikuu cha Leeds nchini Uingereza akiwasilisha
mada kuhusu mfumo wa kilimo cha kisasa kincahozingatia mabadiliko ya
hali ya hewa wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa
kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa
ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini
Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za
Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Huduma za Utafiti na Matumizi ya taarifa za hali ya hewa TMA kutoka
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Ladislaus Chang'a akitoa
maoni wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa
kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa
ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini
Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za
Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wadau wa sekta ya kilimo kutoka, vyuo vikuu, taasisi mbalimbali za
serikali pamoja sekta binafsi walioshiriki hafla ya uzinduzi wa mradi
mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo
wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba akiwa kwenye picha ya pamoja
na washiriki waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na
wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa
ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini
Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za
Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...