Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) pamoja na Jeshi la Polisi Nchini kuratibu safari za mikoani kuanzia Dar Salaam kuondoka saa 11.

Ndiye ameyasema hayo  leo wakati alipofanya ziara katika kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo majira ya saa 10 kuangalia hali ya Usafiri pamoja na changamoto za abiria wanaotumia usafiri wa Mabasi ya Mikoani.

Amesema kuwa Sumatra na Polisi kuratibu kuanza safari saa 11.
Aidha amesema kuwa safari za Dar es Salaam kwenda Dodoma na Dodoma Kwenda Dar es Salaam kwenda masaa 24.

Amesema maagizo hayo yatekelezwe ndani ya wiki mbili ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora ya usafiri kwa Mabasi ya Mikoani.

Amesema kuanza kufanya safari saa 24 Dodoma ni kutaka wananchi kufanya kazi pamoja kuongeza uzalishaji.

Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra Gilliard Ngewe amesema maagizo ya Naibu Waziri ni utekelezaji tu  hakuna maelezo juu ya maagizo hayo.
Amesema usafiri wamejipanga kudhibiti usafiri kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Ndiye akizungumza katika kituo cha Mabasi Ubungo wakati alipofanya ziara majira ya Saa 11alfajili


Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra , Gilliard Ngewe akizungumza akizungumza kuhusiana na Udhibiti wa Usafiri wa Mabasi ya Mikoani

Pics mbalimbali za matukio katika kituo cha Ubungo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...