MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella amewaonya wananchi wa Kijiji cha Kwakibuyu kata ya Kipumbwi wilayani Pangani wanaojishughulisha na uingizwaji wa dawa za kulevya ,wahamiaji haramu na biashara za magendokuacha mara moja vitendo hivyo kabla hawajakumbana na mkono wa sheria huku akiwataka wananchi kuwafichua watu hao.


Eneo la Kipumbwi limekuwa likitajwa kuwa ni miongoni mwa maeneo ambayo kumekuwa bandari bubu ambayo imekuwa ikitumika kwenye matumizi mbalimbali ikiwemo kuingiza bidhaa za magendo, wahamiaji haramu jambo ambalo alisema linapaswa kukomeshwa.

Shigella aliyasema hayo jana wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo kuzungumza na wananchi kwenye mikutano ya hadhara wilayani Pangani ambapo alisema Bandari hiyo bubu zimekuwa tatizo kwenye kutumika kwenye matumizi ambayo yasiyokuwa salama.

“Hapa Kipumbwi mmekuwa na tatizo kubwa la bandari bubu ambayo imekuwa kutumika kwenye matumizi yasiyosalama biashara haramu ya kupitisha wahamiaji, dawa za kulevya ama kusafirisha wahamiaji haramu lakini wapo  baadhi yenu wanadhamira njema ya kuleta bidhaa kutoka maeneo mengine  ikiwemo mkoani Tanga wakati mwengine kivuko kikiwa kimefungwa.
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kwakibuyu Kata ya Kipumbwi wilayani Pangani wakati wa ziara yake ambapo aliwataka kuacha kushiriki kwenye vitendo vya biashara haramu za magendo na uingizaji wa dawa za kulevya.
 Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwl Hassani Nyange akizungumza katika ziara hiyo.
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa wakati wa ziara yake wilayani humo kushoto ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Mbunge wa Jimbo la Pangani  (CCM) Jumaa Aweso.
 Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikilizaa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...