Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu alipowasili kutembelea mradi wa bandari kavu ,Kwala Kibaha Vijiji, Mkoani Pwani
 Meneja wa mradi wa bandari kavu mhandisi Raymond Kweka ,akitoa taarifa ya mradi wakati naibu waziri wa nishati Subira Mgalu hayupo pichani alipotembelea mradi huo.
Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wakazi wa  kijiji cha Mperamumbi Kibaha Vijijini.
Picha na Mwamvua Mwinyi.

NAIBU Waziri wa Nishati,Subira Mgalu ameliagiza shirika la umeme (TANESCO) kuharakisha kufikisha umeme katika mradi mkubwa wa Bandari Kavu ,Kwala Kibaha mkoani Pwani  na wasiwe sehemu ya kuchelewesha mradi huo wa kimkakati wa kitaifa. 

Aidha amesema ,serikali ipo kwenye mpango wa kumpata mkandarasi wa mradi mpya wa Peri Urban ambapo anatarajiwa  kuanza kazi Novemba mwaka huu katika mitaa na vitongoji 182 na zimetengwa sh. bilioni 86 kwa ajili ya kazi hiyo. 

Akizungumza mara baada ya kutembelea ujenzi wa Bandari Kavu na kuongea na wakazi wa Mperamumbi, Kwala na Msua alitaka nishati ya umeme ipatikane wakati mradi ukiendelea hadi ukikamilika. 

Subira alisema, mradi usikwame kwasababu moja wapo nishati anataka nishati ya uhakika ipatikane ili kazi iende haraka .

Alilitaka shirika hilo lijipange vizuri katika maeneo ya miradi mikubwa ya kimkakati na uwekezaji na viwanda na ,wakimbizane na  fursa hiyo. 

Subira alifafanua,  anaamini ukikamilika mradi huo sio fursa ya kitaifa bali na Tanesco kwani itakuwa ni mteja wao. 

"Mamilioni yanalala kwenye mradi huo ,mataluma ya reli yameanza kutandazwa kwenye mradi wa standard gauge, kwahiyo Tanesco msije mkawa sababu ya kucheleweshe suala hili "

Akizungumza na wakazi wa ,Msua na Mperamumbi aliwahakikishia kuwa umeme utafika kwenye maeneo hayo kupitia mradi wa Peri Urban. 

Subira aliwataka wakulima na wafugaji kuheshimiana,kuthaminiana na kufanya kazi pamoja .

Aliwaambia penye maendeleo panahitaji amani hivyo makundi hayo yanapaswa kuishi kwa upendo na sio visasi. 

Meneja mradi wa Bandari Kavu, mhandisi Raymond Kweka  alielezea, mkandarasi wa mradi  ni Suma Jkt na msimamizi ni mamlaka ya bandari Tanzania .

Alisema mradi upo kwenye awamu ya kwanza ya kuandaa na kuweka ukuta. 

Kwa upande wake, mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa, alisema, endapo barabara ya lami ikikamilika italeta maendeleo chanya na kukuza uchumi wa Kwala. 

Akielezea kuhusu umeme ,Jumaa alieleza ni hitaji la wengi katika kijiji cha Mperamumbi, kitongoji cha Msua kata ya Kwala ambapo ikisogezwa huduma hiyo wananchi wataanza kuuza na kuhifadhi vitu vya biashsra na matumizi ya nyumbani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...