WAFANYAKAZI wa Benki ya NMB Tanzania jana walijitokeza kufanya usafi pamoja na jamii maeneo mbalimbali Tanzania Bara na Visiwani pamoja na kutoa msaada wa vitu kwa wahitaji na vifaa vya kufanyia usafi katika baadhi ya maeneo.

Kwa jijini Dar es Salaam wafanyakazi hao wakiongozwa na viongozi waandamizi wa benki hiyo walifanya usafi eneo la Coco Beach pamoja na Soko la Samaki la Feri kwa kushirikiana na wananchi waliojitokeza kufanya usafi kwenye maadhimisho ya usafi duniani.

Hata hivyo mbali na kufanya usafi katika Soko la Feri walitoa msaada wa vifaa vya kufanyia usafi katika soko hilo, ikiwa ni kuhamasisha usafi kwa jamii na kuunga mkono shughuli hizo ambazo ni muhimu kwa jamii yoyote.

Akikabidhi vifaa vya kufanyia usafi Soko la Feri, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd alisema huo ni utaratibu wa kawaida wa benki hiyo kujitolea ama msaada au kushiriki moja kwa moja katika shughuli za kijamii ili kujenga ushirikiano kwa jamii wanayoihudumia.

Alisema Soko la Feri linahudumia watu mbalimbali ambao ni wateja wa Benki hiyo hivyo wana kila sababu kusaidia kuboresha huduma katika soko hilo. Vifaa alivyokabidhi kwa uongozi wa Soko hilo mara baada ya kuwasili ni pamoja na mifagio, reki, makoleo, mifuko maalum ya kuhifadhia na kuzolea taka na vifaa vya kujikinga wakati wa kufanya usafi.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (anayekabidhi) pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo akimkabidhi Mtendaji  wa Soko la Samaki Feri, Mkuu Hanje (anayepokea kulia) vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi katika soko hilo. Wafanyakazi wa NMB leo wamejitolea kufanya usafi katika soko hilo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya usafi. 
Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam wakishiriki kufanya usafi katika soko la Feri lililopo jijini Dar es Salaam. 
Wafanyakazi wa Benki ya NMB Mkoa wa Dodoma wakitoa msaada kwenye wodi ya akinamama Kituo cha Afya cha Makole cha jijini Dodoma walipofika hapo mwisho wa wiki kufanya usafi pamoja na kutoa misaada ya vitu mbalimbali. 
Wafanyakazi wa Benki ya NMB Mkoa wa Dodoma wakitoa msaada kwenye wodi ya akinamama Kituo cha Afya cha Makole cha jijini Dodoma walipofika hapo mwisho wa wiki kufanya usafi pamoja na kutoa misaada ya vitu mbalimbali. 
Wafanyakazi wa Benki ya NMB Mkoa wa Dodoma wakitoa msaada kwenye wodi ya akinamama Kituo cha Afya cha Makole cha jijini Dodoma walipofika hapo mwisho wa wiki kufanya usafi pamoja na kutoa misaada ya vitu mbalimbali. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...