NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anastazia Mabula amezitaka taasisi za fedha pamoja na waendelezaji milki binafsi kushirikiana na Serikali ili kutatua changamoto iliyopo ya uhaba wa nyumba na makazi nchini.

Akihutubia katika ufunguzi wa maonyesho ya nyumba yaliyoandaliwa na benki ya NMB jana na kufanyika katika viwanja vya Kambarage jijini Dodoma, Mabula amesema serikali inauhaba wa nyumba za watumishi hususani baada ya serikali kuhamia jijini Dodoma.

Amesemakuwa Tanzania inaupungufu wa nyumba 3,000,000, hivyo ili kutatua changamoto hiyo, kunatakiwa kujenga nyumba zaidi ya laki mbili kila mwaka hivyo hawana budi kuwashirikisha wadau kikamilifu kama benki ya NMB ilikuziba pengo hilo.

Akizungumzia upande wa Dodoma, Mabula amesema mahitaji ni kuwa na nyumba zaidi ya elfu 23 lakini zilizopo ni nyumba 1329 tuhivyo maonyesho hayo yaliyowakutanisha wateja wa benki ya NMB, waendelezaji milki pamoja na wauzaji wa vifaa vya ujenzi yana tija kubwa kwani yanalenga kuiunga mkono serikali katika suala la maendeleo.

“Makazi bora ni haki ya kila mwananchi, na tukiri kuwa tuna changamoto ya uhaba wa nyumba nchini, lakini kupitia maonyesho haya tunaweza kukutana na wadau mbalimbali kama vile taasisi za fedha waendelezaji miliki na pia wauzaji wa vifaavya ujenzi ili kumaliza changamoto hiyo,” Alisema Mabula.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Angelina Mabula akizungumza kwenye ufunguzi wa maonyesho ya Nyumba day yaliyofanyika jana viwanja vya tawi la NMB Kambarage Jijini Dodoma. Benki ya NMB imeandaa siku ya Nyumba maalum kwaajili ya kuwakutanisha wateja wa mikopo ya nyumba wa NMB na makampuni ya ujenzi wa nyumba ambayo benki hiyo inamkataba nayo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Angelina Mabula akitembelea mabanda ya Wadau wa vifaa vya ujenzi kwenye maonyesho ya nyumba day yaliyoandaliwa na Benki ya Nmb Jijini Dodoma jana. Benki ya NMB imeandaa siku ya Nyumba maalum kwaajili ya kuwakutanisha wateja wa mikopo ya nyumba wa NMB na makampuni ya ujenzi wa nyumba ambayo benki hiyo inamkataba nayo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Angelina Mabula akitembelea mabanda ya Wadau wa vifaa vya ujenzi kwenye maonyesho ya nyumba day yaliyoandaliwa na Benki ya Nmb Jijini Dodoma jana. Benki ya NMB imeandaa siku ya Nyumba maalum kwaajili ya kuwakutanisha wateja wa mikopo ya nyumba wa NMB na makampuni ya ujenzi wa nyumba ambayo benki hiyo inamkataba nayo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...