Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amepokea msaada wa dawa na vifaa tiba wenye thamani ya Sh.Bilioni mbili kutoka Serikali ya India.

Msaada huo wa dawa na vifaa tiba wa Serikali ya India umekabidhiwa kwa Waziri Mwalimu na Balozi wa India nchini Tanzania na kwamba dawa na vifaa tiba hivyo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imedhamiria kuboresha sekta ya afya.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa msaada huo Waziri Mwalimu ameishukuru Serikali ya India kwa kutoa msaada huo ambao umetokana na ombi la Rais Dk.John Magufuli kwa Waziri Mkuu wa India ambaye alikuja nchini.

"Wakati Waziri Mkuu wa India alipokuja nchini,Rais Dk.John Magufuli alitoa ombi la kuomba dawa muhimu na vifaa tiba.Hivyo tunatoa shukrani kwa Serikali ya India kwa msaada huu.Tunatoa shukrani kwa Waziri Mkuu wa India," amesema Waziri Mwalimu.

Akizungumzia zaidi msaada huo,Waziri Mwalim amesema miongoni mwa dawa ambazo zimetolewa na Serikali ya India  ni dawa aina ya Amoxline kwa ajili ya watoto na zipo dozi 19800.
Pia kuna dawa ya kuzuia wajawazito kuvuja damu baada ya kujifungua na kwamba kuna dawa za chanjo ya homa ya ini.
Waziri Mwalim amesema kuwa dawa na vifaa tiba vitapelekwa kwenye Hospitali za umma na kwamba pamoja na msaada huo Serikali imefanikiwa kuboresha sekta ya afya ikiwemo ya kuongeza dawa na vifaa tiba.

"Dawa ambazo zimetolewa zitatolewa bure.Hii imedhihirisha mahusiano mazuri kati ya Tanzania na India.Kwa kukumbusha tu baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani tumekuwa tukinunua dawa kutoka viwandani badala ya watu binafsi.

" Tunaomba Balozi wa India uendelee kuhamasisha wawekezaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba waliopo India kuja kuwekeza nchini kwa kujenga viwanda vya dawa,"amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Wakati huo huo Waziri Mwalimu amezungumzia namna ambavyo Serikali imefanikiwa kuongeza dawa muhimu nchini ambazo kwa sasa zipo za kutosha.

Amefafanua  kuwa taarifa ya Bohari ya Dawa nchini(MSD) ni kwamba kuna ongezeko kubwa la  dawa muhimu hadi  kufikia asilimia 85 kutoka asilimia 36 huko nyuma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...