Na Mwandishi wetu,
Benki ya Biashara ya Mkombozi imezindua rasmi Tawi la Tegeta Jijini Dar es Salaam baada ya tawi hilo kupanda hadhi kutoka kituo cha huduma za fedha na sasa kuwa tawi kamili.

Tawi hilo lilifunguliwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mhashamu Eusebius Nzigilwa katika hafla iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali, wafanyakazi na wateja wa Benki ya Biashara ya Mkombozi.

Akizindua tawi hilo jipya, Askofu Nzigilwa alisema benki inaendelea kukua vizuri kama ilivyotarajiwa na kwamba malengo ya Benki ya Biashara ya Mkombozi ni kuwa na matawi nchi nzima ili Watanzania wote waweze kupata huduma za kibenki.

“Nachukua fursa hii kuwaomba Watanzania wote kuitumia  benki hii. Hii ni benki  inayomilikiwa na Watanzania wenyewe kwani mpaka sasa hakuna pesa yeyote iliyowekwa na mwekezaji yeyote wa nje,” alisema na kuongeza kuwa ufunguzi  wa tawi hilo la Tegeta ni udhihirisho wa dhamira njema ya Benki ya Mkombozi kama mdau muhimu katika uchumi na maendeleo ya sekta ya fedha.

Askofu huyo pia alitoa witokwa Serikali kuendelea kuunga mkono mipango hii ya maendeleo kwani yote hii ipo kwa ajili ya kuwahudumia Watanzania.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya Mkombozi Bw. George Shumbusho alisema kituo cha huduma Tegeta kilifunguliwa  tangu tarehe 23 Julai 2016 na kimepata mafanikio ya kuridhisha katika kipindi hiki kifupi na hata kupata hadhi ya kuwa tawi.
 Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mhashamu Eusebius Nzigilwa akijaza fomu ya kuweka fedha wakati wa uzinduzi wa Tawi la Tegeta Jijini Dar es Salaam.
 Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mhashamu Eusebius Nzigilwa akikata utepe kuzindua Tawi la Tegeta Jijini Dar es Salaam huku viongozi wa benki hiyo wakishuhudia tukio hilo. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya Mkombozi, Bw . George Shumbusho akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi la Tegeta Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya Mkombozi Profesa Marcelina Chijoriga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi la Tegeta Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya Mkombozi wakifuatilia kwa umakini wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tawi la Tegeta Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...