NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR. 

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amewatahadharisha wanachama wa chama hicho, kuwa makini kwa kuepuka propaganda na njama chafu zinazofanywa na viongozi wakuu wa CUF waliotengeneza migogoro bandia ili waweze kupata huruma ya wananchi kuingia madarakani. 

Tahadhari hiyo aliitoa wakati akimnadi mgombea wa nafasi ya Uwakilishi kwa tiketi ya CCM Ramadhan Hamza Chande katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jang’ombe huko katika Uwanja wa Kwaalinatu. Alisema CUF wametengeneza mgogoro bandia wenye lengo la kuiyumbisha CCM mwaka 2020 mbinu dhaifu ambazo hazitoweza kufanikiwa mbele ya CCM ya sasa iliyokuwa imara na inayokwenda sambamba na ulimwengu wa siasa za Kisayansi. 

Dk. Mabodi alisema ushahidi pekee wa kuonyesha kuwa viongozi wa CUF hawana uadui kwa upande wa Zanzibar na Tanzania bara ni pale waliposhirikiana kumnadi mgombea wa Chama hicho katika kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Liwale ambao mgombea wa CCM ameibuka mshindi. Akimnadi na kumuombea kura Mgombea wa CCM katika Uchaguzi wa mdogo wa Jimbo la Jang’ombe Ramadhan Hamza Chande, Dk. Mabodi aliwasihi Wana-CCM na wananchi wa Jimbo hilo kumchagua mgombe huyo ili aendeleze mambo mema yaliyoasisiwa na viongozi wa waliopita wa nafasi hiyo. Alisema CCM imempitisha Ramadhan ikiamini kuwa ana uwezo na anafaa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa kasi kubwa. 

“Mgombea huyo ni mbunifu, mchapakazi na mwenye uzalendo wa kweli nakuombeni wananchi wa Jang’ombe mfanye maamuzi sahihi ya kumpa kura nyingi za ndio aweze kuwatumikia kwa uadilifu. 
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Saadalla ‘Mabodi’ (kulia), akimnadi na kumuombea kura mgombea wa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jang’ombe Ramadhan Hamza Chande(kushoto) katika kampeni za CCM Uchaguzi wa Jang’ombe zilizofanyika Uwanja wa Kwaalinatu.
BAADHI ya Wana –CCM walioudhuria katika Mkutano huo wa kampeni uliofanyika Kwaalinatu.
Mgombea uwakilishi wa CCM Jimbo la Jang’ombe Ramadhan Hamza Chande akiomba kura kupitia mkutano huo wa kampeni uliofanyika uwanja wa Kwaalinatu.
MKE wa Rais mstaafu wa awamu ya nne ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete akimuombea kura Mgombea wa tiketi ya CCM Uchaguzi wa Jang’ombe Ramadhan Hamza Chande. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...