MKEMIA Mkuu wa Serikali, Dkt Fidelice Mafumiko leo amefungua semina ya wadau wa uhifadhi, udhibiti na usimamizi wa kemikali hatarishi hapa nchini.


Akizungumza na wadau hao jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa semina hiyo inatawakumbusha na kuwajenge uwezo wadau wa usimamizi na udhibiti wa kemikali hapa nchini katika kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2003.

Pia amewaasa kutunza na kusimamia kwa usalama kemikali hatarishi ambazo zinaweza kuleta madhara kwa binadamu na mazingira ndani ya bandari. 

“Nawasihi msikilize kwa makini mafunzo haya ili utakapoanza kwenda kwenye utekelezaji wa matakwa ya Sheria na kanuni zake na sio kwa hiari yako. 
Kuna vifungu vya sheria ambavyo vinahusu kuwajibika pale utakapoenda kinyume chake. Sheria inaainisha wajibu na majukumu ya kuhifadhi kwa usalama mnapaswa kuwa makini na kuelewa majukumu na wajibu wenu". amesema Dkt. Mafumiko
Mkemia Mkuu wa Serikali,Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kuufungua semina ya mafunzo ya wa wadau mbalimbali wa usimamizi na udhibiti wa kemikali hatarishi hapa nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi na udhibiti wa kemikali, Daniel Ndiyo akizungumza wakati wa kuufungua semina ya mafunzo ya wa wadau mbalimbali wa usimamizi na udhibiti wa kemikali hapa nchini.
Baadhi wadau wakiwa katika mafunzo ya wa wadau mbalimbali wa usimamizi na udhibiti wa kemikali hapa nchini. 
Mkemia Mkuu wa Serikali, Fidelice Mafumiko akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua semina ya wadau wa uhifadhi usimamizi na udhibiti wa kemikali hapa nchini.

Picha na Avila Kakingo,Globu ya jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...